Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Afungua Skuli ya Msingi ya Ghorofa ya Abeid Amani Karume Mwera
Mar 12, 2025
Rais Dkt. Mwinyi Afungua Skuli ya Msingi ya Ghorofa ya Abeid Amani Karume Mwera
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhamed Mussa (kushoto) ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, ufunguzi huo ulifanyika leo 12-3-2025, Kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud
Na Ikulu - Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Unguja, ufunguzi huo ulifanyika leo 12-3-2025. Kulia kwa Rais ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Muhammed Mussa na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisoma vitabu wakati akiwa katika chumba cha Maktaba ya Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume Mwera Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kuifungua leo 12-3-2025.akiwa na Wanafunzi wa Skuli ya Msingi Mwera wajisomea vitabu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mwanafunzi Adam Simai Uwesu wa Darasa la Sita Skuli ya Msingi Mwera wakati akitoa maelezo ya matumizi ya vifaa vya maabara wakati akitembelea maabara ya Skuli ya Msingi ya Abeid Amani Karume leo 12-3-2025 baada ya kuifungua

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi