Rais Dkt. Mwinyi Akutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa Kuhusu “Generation Equality Forum”
Jun 15, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu “Generation Equality Forum” Mhe. Angela Kairuki, akitoa maelezo ya Kazi ya Kamati hiyo wakati wa mazungumzo yao yalioyfanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake walipofika kujitambulisha leo 15-6-2022, (kulia kwake) Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Mgeni Hassan Juma
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu”Generation Equality Forum, ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe Angela Kairuki (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo 15-6-2022, walipofika Ikulu kwa mazungumzo na kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kamati ya Ushauri ya Taifa kuhusu “Generation Equality Forum” baada ya kumaliza mazungumzo yao walipofika Ikulu Zanzibar leo.