Rais Dkt. Mwinyi Akutana na Kuzungumza na Kamati ya Sheria Mpya ya Makadhi Zanzibar, pia Akutana na TAEC
Sep 12, 2022
Na
Jacquiline Mrisho
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Kamati ya Sheria Mpya ya Makadhi Zanzibar, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 12-9-2022 na (kulia kwa Rais) ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla na Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali.
Mkurugenzi wa Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Simon Petro (katikati) alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo wakati walipokutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kutoa taarifa ya utekelezaji wa Bodi hiyo leo.[Picha na Ikulu] 12/09/2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kulia) akizungumza na ujumbe wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Joseph John Msambichaka (wa pili kulia) walipofika kujitambulisha na kutoa taarifa ya utekelezaji wake Ikulu Jijini Zanzibar leo (kushoto) ni Waziri wa Afya, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Simon Petro (wa pili kushoto) alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Tume hiyo katika ukumbi wa Ikulu Jijin Zanzibar leo.