Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Mwinyi Afungua Mkutano wa Kimataifa wa IDA 20
Dec 07, 2023
Rais Dkt. Mwinyi Afungua Mkutano wa Kimataifa wa IDA 20
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Benki ya Dunia, Mhe. Ajay Banga, alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar leo 6-12-2023 kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wakati wa Mzunguko wa 20 wa Mapitio ya Benki ya Dunia (IDA20) na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum.
Na Administrator

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akielekea katika ukumbi wa mkutano katika Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 6-12-2023 kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda wakati wa Mzunguko wa 20 wa Mapitio ya Benki ya Dunia (IDA 20) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na kulia kwa Rais ni Rais wa Benki ya Dunia, Mhe. Ajay Banga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Fedha na Mipango Tanzani, Mhe. Dkt. Mwingulu Nchemba na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.

 

Washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda Wakati wa Mzunguko wa 20 wa Mapitio ya Benki ya Dunia (IDA20) wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati akifungua mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 6-12-2023 , akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuufungua Mkutano wa Kimataifa wa Tathimini ya Muda,Wakati wa Mzunguko wa 20 wa Mapitio ya Benki ya Dunia (IDA20) akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan unaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja Jijini Zanzibar leo 6-12-2023.

 

 

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi