Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Awasili Zimbabwe kwa Ziara ya Kikazi
May 28, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.[/caption]  

[caption id="attachment_43577" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakipokea zawadi za maua kutoka kwa watoto wa Zimbabwe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.[/caption]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo anafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe, Mhe. Rais Magufuli amepokelewa rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Rais Mnangagwa kisha kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na kupigiwa mizinga 21.

Baadaye leo, Mhe. Rais Magufuli atakuwa na mazungumzo ya falagha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Munangagwa na kisha atahudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Mnangagwa kwa heshima yake.

[caption id="" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakiwa wamesimama wakati nyimbo za taifa la Tanzania na Zimbabwe zilipokuwa zikipigwa mara baada ya kuwasili nchini Zimbabwe.[/caption]  
[caption id="attachment_43582" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.[/caption]

Kesho, Mhe. Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake na kisha atatembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa wa ukombozi wa Zimbabwe.

Katika ziara hii Mhe. Rais Magufuli ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Ndg. Philip Mangula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

28 Mei, 2019

Habari Mpya

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi