Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Rais Dkt. Magufuli Aitangaza Dodoma kuwa Jiji.
Apr 26, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_30932" align="aligncenter" width="900"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano huo .

[/caption] [caption id="attachment_30940" align="aligncenter" width="900"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na Usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma katika uwanja wa Jamhuri ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano .[/caption] [caption id="attachment_30937" align="aligncenter" width="874"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akielekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na Usalama wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano .[/caption]

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza rasmi kwa mamlaka aliyonayo kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Mkoani Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyoadhimishwa Uwanja wa Jamhuri mkoani humo.

“Tuliona Dar es Salaam ilivyokuwa makao makuu kipindi hicho na ilikuwa inaitwa Jiji, nikaona niangalie katika nchi yetu kuna Majiji mangapi, tuna Manispaa ngapi, Halmashauri ngapi na mimi nina mamlaka gani katika kutengeneza Majiji au Manispaa, nikakuta Dar es Salaam ni Jiji, Tanga ni Jiji, Arusha ni Jiji, Mwanza ni Jiji, Mbeya ni Jiji nikaambiwa Dodoma ni Manispaa nikasema hili haliwezekani kwa hiyo kuanzia leo kwa mamlaka waliyonipa Watanzania Dodoma ni Jiji”

[caption id="attachment_30930" align="aligncenter" width="900"] Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano katikati ni katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.[/caption] [caption id="attachment_30938" align="aligncenter" width="849"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akipokea heshima ya Kupigiwa mizinga 21 wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano[/caption]

“Kwa hiyo maandalizi yote ya kisheria lazima yaanze sasa kufanyika na huyu Mkurugenzi aliyekuwa wa Manispaa hapa hapa leo anakuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na hili litakuwa Jiji la peke yake kwa sababu lipo katikati ya Tanzania” ameongeza Dkt. Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli amesema kuwa anatarajia kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Ayodeji Adesina ambao wanafadhili miradi 25 hapa nchini yenye thamani ya Dola Bilioni 1.986, ili kati ya miradi mbalimbali atakayoongea, Dodoma ipewa kipaumbele kama Jiji.

Akizungumzia kuhusu miaka 54 ya Muungano Rais Magufuli amesema kuwa, Tanzania imekuwa na mafanikio mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa maeneo ya ushirikiano, ambapo mwaka 1964 yalikuwa maeneo 11 na sasa yapo maeneo 22, Muungano umefanya  nchi imekuwa na sauti na kujiamini, vile vile kutoa mchango katika masuala mbalimbali ya Kimataifa na kusuluhisha migogoro.

[caption id="attachment_30941" align="aligncenter" width="900"] Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Jaji mkuu wa Zanzibar Mhe. Othuman Makungu wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano.[/caption] [caption id="attachment_30931" align="aligncenter" width="900"] Sehemu ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano huo.[/caption] [caption id="attachment_30934" align="aligncenter" width="856"] Kikosi maalum cha magereza kikionesha umahiri wake katika kuruka kikwazo cha moto.[/caption] [caption id="attachment_30935" align="aligncenter" width="900"] Kikosi cha Komando wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari kwa meno wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema leo mkoani Dodoma ikiwa ni miaka 54 tangu kuasisiwa kwa muungano.[/caption] [caption id="attachment_30936" align="aligncenter" width="900"] Gwaride la askari wa Vikosi vya ulinzi na Usalama wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kutoa heshima wakati wa madhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanziabar.[/caption]

Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka Wananchi kulinda na kuudumisha Muungano uliopo na kutoa ushiririkiano kwa vyombo vya usalama kwani Muungano huo ni tunu kwa Taifa.

“Kikubwa kwa Watanzania bila kujali dini, kabila, vyama tusimame imara, tutunze na kuusimamia huu Muungano kwa nguvu zetu zote, Serikali ninayoiongoza na Serikali ya Zanzibar tupo imara, Muungano huu tutaulinda kwa nguvu zote, tutautunza na kuusimamia” amesisitiza Dkt. Magufuli.

Tanzania imeadhimisha Sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibari ambapo Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Muungano wetu ni wa mfano Duniani tuuenzi, tuulinde, tuuimarishe na kuudumisha kwa maendeleo ya Taifa letu

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi