[caption id="attachment_35844" align="aligncenter" width="750"] Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.[/caption]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Septemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjukuu wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Prince William (Duke of Cambridge) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo Prince William ameelezea kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza, na amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata nafasi ya kuzungumza nae.
Prince William amezungumzia juhudi anazozifanya katika uhifadhi wa wanyamapori na amemuomba Mhe. Rais Magufuli kuendelea kushirikiana katika kukabiliana na vitendo vya ujangili hasa wa Tembo.
[caption id="attachment_35846" align="aligncenter" width="750"]Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemkaribisha Prince William kuja hapa Tanzania wakati wowote, na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Uingereza ikiwemo kushirikiana nae kuhifadhi wanyamapori.
“Naomba ufikishe salamu zangu kwa Malkia Elizabeth II, mwambie Watanzania tunaipenda Uingereza na tutaendeleza na kuuimarisha zaidi ushirikiano wetu mzuri kwa manufaa yetu sote” amesema Mhe. Rais Magufuli.
[caption id="attachment_35847" align="aligncenter" width="750"]Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imefanya juhudi kubwa za kukabiliana na ujangili hasa wa Tembo ambapo kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kwamba anatarajia Prince William ataunga mkono ili kukomesha kabisa ujangili katika hifadhi zote za wanyamapori hapa nchini.
Prince William aliyeingia hapa nchini jana atakuwepo kwa siku 4 hadi tarehe 29 Septemba, 2018.
[caption id="attachment_35849" align="aligncenter" width="750"]Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Septemba, 2018