[caption id="attachment_8713" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia kwa makini mafunzo hay oleo Jijini Mbeya. Mafunzo hayo yamelenga kuwa jengea uwezo watumiaji wa mfumo huo katika Halmashauri zote nchini chini ya ufadhili wa USAD Tanzania/PS3.[/caption]
Na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya
Katika kuhakikisha inaongeza nguvu katika usimamizi wa Mifumo yote ya Sekta za Umma iliyofanyiwa maboresho PS3 imejipanga kuwajengea uwezo watumiaji wa mifumo hiyo katika eneo la usimamizi ili ifanyekazi kwa ufanisi na kuwa endelevu hata mara baada ya Program hiyo kumaliza muda wake ifikapo 2020.
Hayo yamebainishwa leo na Mkuu wa Timu ya Fedha kutoka Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dkt. Gemini Mtei alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi wakati wa mafunzo kwa ajili ya watumiaji wa Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Serikali za Mitaa (PlanRep) Jijini Mbeya leo.
[caption id="attachment_8714" align="aligncenter" width="750"]Dkt. Gemini amesema kuwa mpaka sasa wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho katika mifumo mbalimbali iliyokuwa inatumika na Serikali na kuongeza kuwa jambo kubwa la kutilia mkazo kwa sasa ni juu ya namna ambavyo mifumo hiyo itasimamiwa ili iwe endelevu.
“Jambo ambalo sasa tunatarajia kulitilia mkazo zaidi ni eneo la usimamizi wa mifumo ya sekta za umma, tunataka kuona mifumo hii ikiendelea hata baada ya Programu yetu ya PS3 itakapomaliza muda wake,” alisema Dkt. Gemini.
[caption id="attachment_8716" align="aligncenter" width="750"]Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa usimamizi wa mifumo PS3 iliona haja ya kuendelea na mifumo iliyokuwepo badala ya kuja na mifumo mipya jambo ambalo limewezesha Serikali kuendelea kuwa msimamizi wa karibu wa mifumo hiyo.
Akizungumzia mafunzo hayo ya Mfumo mpya wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep), Dkt. Gemini amesema kuwa mfumo huo ni matokeo ya changamoto zilizoanishwa na watumiaji (wafanyakazi wa serikali) ambao walibainisha maeneo ambayo wangependa yafanyiwe maboresho.
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali fedha itokanayo na mchakato mzima wa uandaaji wa bajeti uanzia ngazi ya kijiji ambapo inahusisha rasilimali watu ambao wote wanahitaji kugharamiwa.
[caption id="attachment_8722" align="aligncenter" width="750"]Dkt. Gemini anesema kuwa baada ya kuainishwa kwa changamoto hizo TAMISEMI walikuja na mapendekezo ya kuufanyia maboresho mfumo huo ambao umekuja kutatua changamoto hizo ikiwemo kupunguza gharama kwa kurahisha mawasiliano kwa njia ya Kielekroniki badala ya mtu kufunga safari kutoka sehemu moja hadi nyingine, lakini pia kupitia mfumo huo mtumiaji ataweza kufanya marekebisho ya Bajeti yake au taarifa yake bila ya kuchapisha nakala yote jambo linaloondoa gharama.
Kwa upande wake Mtaalamu wa Masuala ya Tehama kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI James Mtatifikolo amesema kuwa Serikali kupitia OR – TAMISEMI ndiyo yenye dhamana ya kuisimamia mifumo hiyo baada ya kujengewa uwezo na PS3.
Mtatifikolo aliongeza kuwa maboresho hayo ya mifumo hasa wa Uandaaji wa Mipango na Bajeti (PlanRep) ni kwamujibu wa mahitaji ya Sera ya Tehama na miongozo mbalimbali ya Serikali.
Pamoja na kuwa mradi wa huu PS3 unatekelezwa katika Mikoa 13 na Halmashauri 93 za Tanzania Bara bado manufaa yake yanazifikia Halmashauri zote kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa.
Katika muendelezo wa kuwajengea uwezo watumiaji wa Mifumo iliyofanyiwa maboresho Serikali kwa kushirikiana na USAID Tanzania/PS3 wanaendesha mafunzo ya nchi nzima ambapo yanawashirikisha watumiaji wa mifumo ya PlanRep na Mfumo wa Fedha (FFARS) ambapo washriki watano kutokoa Halmashauri 185 na wane kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.