Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwarobaini Utoaji Huduma za Afya Wapatikana
Apr 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya.

Serikali inaendelea na mikakati wa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora za afya na kwa wakati ili kuleta ustawi katika kufikia azma ya Tanzania ya viwanda.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Mbeya na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi alipokuwa akizinduzi mafunzo kwa wakufunzi wa kitaifa kuhusu Bima ya Afya ya Jamii (CHF), mfumo wa kupeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma (DHFF), na mfumo wa manunuzi ya dawa nje ya mfumo wa kawaida wa MSD (Jazia – Prime Vendor System).

Kaimu Katibu Tawala huyo aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya ya uhakika kwa kupata huduma bora za afya na kwa wakati, jambo lililopelekea kuanzishwa kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma.

[caption id="attachment_29748" align="aligncenter" width="1000"] Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Constatine Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Mifumo iliyoborehswa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na wa Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3. Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk. Robert Salim, Meneja Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu na Mwakilishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi. Nkinda Shekalage.[/caption] [caption id="attachment_29749" align="aligncenter" width="1000"] Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Janeth Kibambo akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku tano kuhusu Mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na wa Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.[/caption]

Lengo mahususi ya mafunzo haya ni kuelewa kwa upana maana ya ugatuaji wa mipango ya afya na bajeti kwa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma (DHFF)”yenye matarajio ya kupunguza urasimu na kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa  kuimarisha uwajibikaji na uboreshaji wa  uandaaji wa mipango, bajeti na matumizi  yanayolenga kuboresha huduma za afya,” alisisitiza.

Aliongeza kuwa mpaka sasa katika robo ya pili ya mwaka Serikali imekwisha peleka takribani shilingi bilioni 45 katia jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 5,125 nchi nzima.

Aidha Mushi alibainisha kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa afya kwa wananchi imekuwa na mikakati ambayo inashirikiana na wadau wa maendeleo katika kuitekeleza ikiwemo utekelezaji wa maboresho ya mifumo ya sekta za umma inayoratibiwa na TAMISEMI kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la maendeleo USAID/PS3 ambao unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara.

“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau wetu wa maendeleo ambao tumeendelea kushirikiana nao katika Nyanja mbalimbali, kwa kipekee niwashukuru wenzetu wa Wadau wa Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), HPSS, PS3, Global Supply Chain Program, Boresha Afya – Deloitte, World Vision. EGPAF, Jhpiego, GIZ, AGPAHI na Pharmaccess,” aliongeza.

[caption id="attachment_29750" align="aligncenter" width="1000"] Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Bi. Nkinda Shekalage akifafanua juu ya madhumuni ya mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.[/caption] [caption id="attachment_29751" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD, (Jazia - Prime Vendors System) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3.[/caption]

Akitoa muongozo wa mafunzo hayo Mwakilishi kutoka OR- TAMISEM, Bi. Nkinda Shekalage alisema kuwa mafunzo haya yataleta chachu katika kufikia malengo ya utoaji wa huduma za afya zilizo bora na kwa ufanisi endapo washiriki wataenda kutekeleza wajibu wao wa kuwafundishi waliochini yao kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Timu ya Mifumo ya Fedha wa PS3, Dkt. Gemini Mtei alisema kuwa PS3 imeshirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuiunda DHFF kwa ajili ya kuwezesha vituo vya kutolea huduma za afya kupokea fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja(HBF) moja kwa moja kwenye akaunti zao.

Dkt. Gemini alisema kuwa msaada uliotolewa na PS3 ni wa kitaalam, ili kuwezesha kuwepo kwa mfumo mzuri wa upokeaji wa hizi fedha.  Sambamba na hilo, PS3 imeshirikiana na Serikali kuweka mifumo itakayowezesha DHFF kufanikiwa, mifumo hii ni Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa kwenye Vituo vya Kutolea Huduma (FFARS) pamoja na Mfumo wa Mipango, Bajeti na Utoaji wa Taarifa (PlanRep).

[caption id="attachment_29752" align="aligncenter" width="1000"] Baadhi ya wawezeshaji wa mafunzo ya siku tano kuhusu mifumo iliyoboreshwa ya Bima ya Afya ya Jamii (CHF), Ugatuaji wa Fedha na Mipango katika Vituo vya Afya (DHFF) na Manunuzi ya dawa nje ya mfumo rasmi wa MSD(Jazia - Prime Vendors System) wakijadiliana jambo mara baada ya uzinduzi rasmi wa mafuynzo hayo leo Jijini Mbeya. Washiriki wa mafunzo hayo ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Makatibu Afya, Waratibu wa Bima za Afya, Maafisa Ugavi, Maafisa Tehama na Wahasibu kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Katavi, Rukwa na Songwe chini ya ufadhili wa USAID/PS3. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Mbeya.)[/caption]

“Niseme tu kuwa DHFF haiwezi kufanya kazi vizuri endapo hakuna mifumo thabiti ya mipango na bajeti katika ngazi ya kutolea huduma, ndio maana PS3 imesaidia katika hilo, na mifumo hiyo miwili (PlanRep na FFARS) ilizinduliwa mwezi Septemba 2017 na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa”. Alifafanua Dkt. Gemini.

Aliongeza PS3 itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza uimarishwaji wa mifumo mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya afya na sekta nyinginezo, kulingana na mahitaji ya Serikali.

Mradi wa PS3 umesaidia pia kujenga uwezo kwa Serikali katika maeneo ya utekelezwaji wa mpango wa DHFF, CHF iliyoboreshwa, na PV.  USAID kupitia PS3 imewezesha mafunzo ya wakufunzi wa kitaifa yaliyofanyika mjini Morogoro wiki moja iliyopita, na pia ndiyo inayofadhili mafunzo yaliyoanza leo katika mikoa minne: Mbeya, Mwanza, Morogoro na Mtwara.  Mafunzo haya yamehusisha maafisa kutoka mikoa yote iliyo Tanzania bara, na baadaye yatashuka kwenda ngazi ya Halmashauri na kwingineko.

Mafunzo haya yamekuja kufuatia kuanza kwa kubainika kwa changamoto katika utekelezaji wa utaratibu wa kupeleka fedha moja kwa moja kwenye vituo vya kutolea huduma za afya (Direct Health Facility Financing) ili kuzipa nguvu zaidi Kamati za Usimamizi wa Huduma za Afya (HFGC) katika kupanga na kusimamia huduma za Afya katika ngazi ya jamii uamuzi uliotokana na mkutano wa mwaka wa mapitio ya Sekta ya Afya (Joint Annual Health Sector Review) uliofanyika Desemba 7, 2016.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi