Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Profesa Kikula Aongoza Kikao cha Kazi Tume ya Madini
Dec 21, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_39145" align="aligncenter" width="750"] Kamishna kutoka Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma (kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha Tume ya Madini kilichofanyika Desemba 21, 2018 jijini Dodoma. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula.[/caption]

Leo tarehe 21 Desemba, 2018 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ameongoza kikao cha kazi cha Tume ya Madini kilichofanyika jijini Dodoma. Kikao hicho kilishirikisha makamishna wa Tume ambao ni Mtendaji  Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Nchini (FEMATA), Haroun Kinega, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  Dorothy Mwanyika, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Florence Turuka na  Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa.

Wengine ni Dkt. Athanas Macheyeki, Profesa Abdulkarim Mruma Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya pamoja na watendaji wa Tume ya Madini.

Pamoja na mambo mengine kikao hicho kilijadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya Tume na Mpango Mkakati wa Tume wa miaka mitano (2019/20 -2023/2024). Katika kikao hicho kati ya masuala yaliyokubaliwa ni pamoja na leseni ambazo hazifanyiwi kazi kufutwa na tathmini ya kina kufanyika kwa waombaji wa leseni ili kubaini kama wanakidhi vigezo kama vile uwezo wa kifedha na utaalam.

[caption id="attachment_39146" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akifafanua jambo katika kikao hicho[/caption] [caption id="attachment_39147" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi wa Leseni na TEHAMA kutoka Tume ya Madini, Terence Ngole (katikati) akielezea mikakati ya Tume kwenye utoaji wa leseni kwenye kikao hicho. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tume, Julius Moshi na kulia ni Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Dkt. Abdulrahaman Mwanga[/caption] [caption id="attachment_39148" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira kutoka Tume ya Madini, Dkt. Abdulrahaman Mwanga akieleza jambo katika kikao hicho.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi