Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

POSTA Yashiriki Maonyesho ya 21 ya Wajasiriamali wa Afrika Mashariki
Dec 12, 2021
Na Jacquiline Mrisho

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Shirika la Posta Tanzania linashiriki Maonesho ya 21 ya Wajasiriamali wadogo na wa kati wa Afrika Mashariki maarufu kama maonesho ya Nguvu Kazi /Jua Kali yanayofanyika katika viwanja vya Rock City Mall, Jijini Mwanza.

Maonesho haya yalianzishwa kwa lengo la kuwaunganisha wajasiriamali wa Afrika Mashariki ili kubadilishana ujuzi na mbinu mbalimbali za kibiashara. Kwa mwaka huu maonesho haya yanafanyika nchini Tanzania katika Jiji la Mwanza huyu yakibeba kauli mbiu isemayo "Kuhamasisha ubora na uvumbuzi, ili kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wadogo na wakati wa Afrika Mashariki na kuinuka kiuchumi baada ya janga la uviko 19".

Posta imeshiriki maonesho haya kwa kutangaza na kutoa huduma zake mbalimbali hasa za Duka mtandao, Posta kiganjani pamoja na huduma za Usafirishaji.

Maomesho hayo yamehudhuriwa na Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, South Sudan na Tanzania mwenyewe.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi