[caption id="attachment_46405" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Juliana Shonza akikimbia leo Agost 31 kuashiria ufunguzi wa mbio za riadha ya Kondoa Irangi Marathon mwaka 2019 zitakazofanyika Jijini Dodoma.[/caption]
Na Shamimu Nyaki –WHUSM DODOMA
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa watanzania wanao wajibu wa kulinda,kuthamini na kuendeleza Utamaduni wa nchi katika shughuli zote za uzalishaji pamoja na za kijamii.
Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa maonyesho ya Utalii wa Utamaduni, mambo kale na bidhaa za asili za hapa nchini yaliyoongozwa na kauli mbiu “Utamaduni mambo kale na bidhaa za asili yetu ni fursa ya kibiashara katika utalii” ambayo yalikuwa na lengo la kutangaza utalii wa utamaduni .
[caption id="attachment_46406" align="aligncenter" width="1000"]Naibu Waziri Shonza ameeleza kuwa lengo la matamasha ya Utamaduni ni kutangaza utamaduni wa nchi yetu unaojumuisha vitu mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili,ngoma za asili,bidhaa za asili chakula pamoja na mila na desturi za jamii zetu.
“Hatuwezi kuwa na Taifa ambalo halienzi Utamaduni wake pamoja na lugha yake ya asili ya Kiswahili ambayo sasa ni lugha ya nne ya mawasaliano katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) hivyo watanzania ni lazima tuwe mstari wa mbele katika kuuthamini utamaduni wetu” Mhe.Shonza.
Awali akifungua mashindano ya riadha ya Kondoa Irangi Marathon Mhe.Shonza amesema kuwa michezo inasaidia kuibua vipaji ambapo amewataka wananchi wa Jiji la Dodoma kuwa mstari wa mbele katika kushiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Jijini hapo kwakua ndio wenyeji wa Makao makuu ya nchi hivyo wasiwaachie wageni pekee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Yakwetu Fair Dodoma Bw.Japhet Jackson ambaye ndio mratibu wa maonyesho hayo amesema kuwa lengo la kufanya maonyesho hayo ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kuutangaza Mkoa wa Dodoma kama Makao Makuu ya nchi pamoja na kutangaza fursa zilizopo ili kuvutia watalii wengi na wawekezaji kufka Jijini hapo.
Bw.Japhet Jackson ameongeza kuwa maonyesho hayo yatakuwa endelevu ambayo yatafayika kila mwaka na yatalenga kutangaza utalii wa utamaduni pamoja na vivutio vya asili vilivyopo mikoa ya kusini ambayo imekuwa haitangazwi vizuri ikiwemo kimondo cha mbozi,mto ruaha,kitulo na mbuga ya Selous.
“Maonyesho haya yanalenga kuwainua wafanyabiashara wa bidhaa za Utalii na Utamaduni ambazo zinatangaza nchi yetu kutokana na upekee wa bidhaa hizo”alisema Bw.Japhet.
Naye mshiriki wa maonesho hayo Bw.Emmanuel John amesema maonyesho hayo yamewapa fursa ya kutangaz bidhaa zao pamoja na kupata nafasi ya kufika Jiji la Dodoma mbalo kwa sasa ndio makao makuu ya Serikali.
Maonyesho hayo yamefanyika kuanzia Agosti 21 na yamehitimishwa leo Agosti 31 ambapo baadhi ya shughuli za kiutamaduni zilifanyika ikiwemo kuonyesha mavazi ya asili,ngoma za asili michezo ya jadi na shuguli nyingine za utamaduni.