[caption id="attachment_41941" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mama Anne Makinda akitoa salaam za Bodi wakati wa uzinduzi wa huduma hizo.[/caption]
[caption id="attachment_41940" align="aligncenter" width="750"]
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akitoa maelezo ya awali wakati wa uzinduzi wa mpango huo katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia[/caption]
Na Mwandishi Wetu
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umezindua rasmi huduma za Mkoba za Madaktari Bingwa Wilayani Mafia Mkoani Pwani ambazo zitaendelea kwa wiki nzima katika hospitali ya Wilaya ya Mafia.
Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amesema mpango huu ni mwendelezo wa mkakati wa Mfuko huu kufikia wananchi na huduma za madaktari bingwa katika maeneo ambayo yana uhaba wa madaktari hao.
Amesema Mfuko kwa nyakati tofauti umeshafikia mikoa 17 na huduma hizo za mkoba za madaktari bingwa ambayo ni Rukwa, Lindi, Kigoma, Pwani, Mara, Tabora, Manyara, Mtwara, Shinyanga, Simiyu, Kagera, Singida, Ruvuma, Iringa, Njombe, Geita na Katavi. Kati ya hiyo mikoa 6 imeshafikiwa na mara mbili.
"Tumeona hitaji la huduma hizi huku Mafia na kwa kushirikiana na Hospitali ya Wilaya hapa Mafia zoezi hili litaendelea kwa wiki nzima kwa kila mwananchi mwenye hitaji la huduma za madaktari hawa ambao wametoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili" alisema Bw. Konga
[caption id="attachment_41942" align="aligncenter" width="750"]Akifungua huduma hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Mhe. Shaibu Nunduma ameipongeza NHIF kwa kuleta huduma hii Mafia.
"Asilimia kubwa ya wagonjwa wetu hawana uwezo wa kuzifuata huduma za madaktari bingwa huko walipo na kwa idadi ya wataalam waliopo hapa Mafia tusingeweza kuhudumia wananchi wa mafia ambao wako 53,083 hivyo naishukuru sana NHIF kwa kutuletea huduma hizi"Amesema Mhe. Shaibu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mhe. Anne Makinda amesema Serikali yetu imeweka mkazo mkubwa katika afya na bajeti ya dawa kwa sasa imeongezeka hadi kufikia takriban bilion 300. Amesema lengo la Serikali yetu ni kila mtu kuwa na bima ya afya na katika kutimiza azma hii, Mfuko huu unalengo la kufikia 50% ya wananchi mwakani 2020.
[caption id="attachment_41939" align="aligncenter" width="750"]"Lengo letu ni kuwa na watu wenye bima ya afya wakiwa wazima maana itakuja siku ambayo ugonjwa unakujia ghafla na huna fedha. Mfuko huu unamwezesha hata mtoto wako kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka kwa Sh. 50,400 wakati kwa wakulima Sh. 76,800 kwa kwa mwaka" amesema Mhe. Makinda
Kwa upande wao wananchi wa Mafia ambao walifika kwa wingi kupata huduma za Madaktari Bingwa hao kutoka Hospitali ya Muhimbili wameushukuru Mfuko kwa huduma hizo na wameonesha kuhamasika kuitumia fursa hiyo.