Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri wa Madini Atembelea Banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Sabasaba
Jul 13, 2020
Na Msemaji Mkuu

Leo tarehe 13 Julai, 2020 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametembelea Banda la Tume ya Madini na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Saalaam.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini imejipanga kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wawe na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Sekta ya Madini.

Akielezea mikakati ya Serikali katika kuhakikisha Sekta ya Madini inakua zaidi amesema kuwa ni pamoja na kuhakikisha madini ghafi yanaongezewa thamani nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi hivyo kuongeza ajira kwa watanzania.

“Kama Serikali tunataka kuhakikisha kuanzia mchimbaji, mchenjuaji, mwongeza thamani hadi mfanyabiashara wa madini ananufaika pamoja na watoa huduma kwenye shughuli za uchimbaji wa madini,” amesema Naibu Waziri Nyongo.

Katika hatua nyingine Nyongo amewataka wachimbaji wa madini kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi