Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu  Waziri Shonza: Wanatasnia ya Filamu Rasimisheni Kazi Zenu
Jan 24, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_50369" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na Wadau wa Tasnia ya Filamu wa Mkoa wa Singida.[/caption]

Na Anitha Jonas – WHUSM

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewasisitiza wanatasnia ya filamu kuhakikisha wanarasimisha kazi zao na kujisajili.

Mhe. Shonza ametoa  agizo  hiyo  leo  mkoani  Singida alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kutaka kusikiliza kero zao na kuwaeleza wadau hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo,kuthibiti uharamia ili kuhakikisha wanafaidika na kazi zao.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wanatasnia hao wa filamu kuzingatia suala la uandaaji wa muswada wa filamu na kupeleka miswada hiyo kwa maafisa utamaduni  kwa ajili ya ukaguzi na kupata ushauri wa filamu watakayoandaa  sababu hiyo ni moja ya njia itakayosaidia kuandaa kazi zenye ubora.

“Kwanza ningependa niwashauri muache kusambaza au kuuza kazi zenu kwa njia ya ‘flash’ katika vibanda vya kuuza filamu sababu hii bado ni njia inayowakandamiza na hauwezi kupata faida ya kazi yako, sasa hivi kazi hizo za filamu zinasambazwa kwa mfumo wa kidigitali mfano kwenye Swahilifilx na Netflix,kikubwa ni kazi yako iwe yenye ubora na iliyozingatia utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa filamu ikiwemo wachezaji  kuvaa uhusika na kucheza katika maeneo yenye uhalisia wa filamu hiyo,”alisema Mhe.Shonza.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo alisema bodi  imekuwa ikitoa mafunzo kwa wadau wa tasnia hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandaa kazi bora zitakazo kuwa na ushindani  kwa  ndani na nje ya nchi  na kwa hivi karibuni wanatarajia kufanya mafunzo hayo mkoani Dodoma na kwa wadau wa Singida ambao hawajawahi kupata mafunzo hayo wanakaribishwa kushiriki.

“Bodi ya filamu katika kuimarisha masoko ya usambazaji wa filamu ndani na nje ya nchi imempata mdau kutoka Nigeria  mwenye Kampuni iitwayo ENVIVO ambaye yupo tayari  kununua jumla kazi mia moja mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu,zenye hadithi mbalimbali za kitanzania ambapo zitatafsiriwa kwa lugha kwa lugha ya Yoruba,Pijini  na Igbo kusambazwa,kikubwa katika kazi hizo ni ziwe zimebeba hadithi za kitanzania na zenye ubora na pia ziwezinaendana na  muswada,”alisema Dkt.Kilonzo.

Pamoja na hayo Dkt.Kilonzo aliwasihii wadau hao kuwa mfumo wa usambazajiwa kwa kazi za filamu kwa sasa umebadilika na filamu kwa sasa mara baada ya kukamilika inafanyiwa uzinduzi katika majumba ya sinema na huko itaonyeshwa kwa kipindi fulani na baadae inapelekwa katika mifumo mingine ya kidigitali na hatua ya kuiweka katika CD na Youtube niyamwisho hii ni katika kulinda kazi hizo na uharamia pia kuhakikisha msanii anapata faida ya kazi yake.

Kwa upande wa Afisa Utamaduni Mkoa Bw.Hendry Kapera alisema wasanii wengi wa filamu katika mkoa huo hawataki kujisajili wala kurasimisha kazi zao hii ni changamoto kubwa na wamekuwa wakijiweka mbali na maafisa utamaduni wa wakihofia kuulizwa kuhusu usajili na hii imechangia wao kuandaa kazi zisizo na ubora sababu hawapendi kushirikiana na maafisa hao.

Halikadhilika nae mmoja ya wasanii hao wa filamu kutoka Wilaya ya Ikungi  Bw.Salumu Ntandu aliomba bodi ya filamu kuwapatia mafunzo wadau hao wa mkoa huo na pia aliwasihii wasanii wenzake kuwa na umoja na kuacha migogoro kwani umoja wao ndiyo utakaoweza kutangaza kazi zao na kutangaza mkoa wao pale watakapo andaa kazi nzuri zenye ubora na kushirikishana katika kuitangaza na  kuizindua.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi