Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Shonza Awataka Waalimu wa Michezo Kupata Mafunzo Katika Chuo cha Michezo Malya.
Jul 24, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45700" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) Julai 23,2019 wakati wa alipofungua wa mashindano ya mpira wa wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro.[/caption]

Na: Shamimu Nyaki –WHUSM MOROGORO

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka waalimu wote wa michezo mbalimbali kujiunga na Chuo cha Michezo Malya kilichopo Jijini Mwanza ili kupata mafunzo ya muda mrefu na mfupi yanayotolewa chuoni hapo kwa lengo la kupata utaalamu mzuri wa kufundisha michezo hapa nchini.

Mhe.Shonza ameyasema hayo jana Mkoani Morogoro wakati alipofungua mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa ambapo amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu pamoja na TAMISEMI zinashirikiana katika kukuza michezo hapa nchini ikiwemo kuhamasisha walimu wa michezo kuongeza ujuzi unaoendana na wakati katika kufundisha michezo.

[caption id="attachment_45701" align="aligncenter" width="1000"] Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Yahya Hassan akizungumzia mafanikio ya mpira wa Wavu katika mkoa wa Morogoro wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira huo kitaifa yanayofanyika mkoani hapo yaliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kulia) Julai 23,2019.[/caption] [caption id="attachment_45702" align="aligncenter" width="1000"] Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Taifa (TAVA) Bw.Benedito Kambanyuma akitoa historia ya Shirikisho hilo pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mchezo wa Wavu wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira huo kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro yaliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza Julai 23,2019.[/caption]

“Wizara yetu kupitia Chuo cha Michezo Malya inatoa mafunzo ya cheti pamoja na astashahada kwa waalimu wa michezo na wanapomaliza wanakwenda kufundisha michezo katika shule zetu na kwa wanamichezo, hivyo nitoe rai kwa waamuzi pamoja na waalimu ambao hamjapata mafunzo hayo mjiunge na chuo hicho ili kupata ujuzi zaidi wa kufundisha michezo”alisema Mhe.Shonza.

Aidha Mhe.Shonza ameupongeza uongozi wa Shirikisho la mpira wa  Wavu hapa nchini (TAVA) kwa jitihada kubwa uliofanya mpaka kufanikisha ushiriki wa timu za Taifa za Wavu wa ufukweni katika michuano ya Afrika iliyofanyika katika nchi za Kenya,Algeria,Misri pamoja na Cape verde ambapo zimeiletea heshima na kuitangaza vyema nchi.

Vilevile Mhe.Shonza ameihakikishia TAVA pamoja na Vyama vya Michezo vyote hapa nchini kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI kushiriki katika mashindano ya UMITASHUNTA NA UMISETA kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Taifa.

[caption id="attachment_45703" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro Julai 23,2019.[/caption] [caption id="attachment_45704" align="aligncenter" width="1000"] Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Morogoro,viongozi wa Shirikisho la mpira wa Wavu Tanzania pamoja na baadhi ya wachezaji mara baada ya kufungua mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanayofanyika mkoani Morogoro Julai 23,2019.[/caption]

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA) Bw.Benedito Kambanyuma amesema kuwa michuano ya klabu bingwa ya Taifa kwa wanaume na wanawake hufanyika kila mwaka tangu mwaka 2018 ambapo ilianzishwa ligi kupitia vyama vya Mikoa na washindi wanne wa kila mkoa hukutana katika michuano na kupata bingwa wa Taifa.

Bw.Kambanyuma ameongeza kuwa TAVA imeanzisha utaratibu wa kutambua vituo vyote vya timu za watoto ambazo  zitasaidia kupatikana kwa vipaji vingi vya mchezo huo pamoja na kukuza kipato kwa wachezaji.

Naye Mchezaji wa kulipwa anayechezea nchini Rwanda Bw.Jackson Mmari ameeleza kuwa mchezo wa Wavu ni miongoni mwa michezo inayotoa ajira na kukuza kipato ambapo amewashauri vijana kujiunga na mchezo huo ili kupata ajira.

Mashindano ya mpira wa Wavu kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili hapa nchini ambapo timu tisa ikiwemo Jeshi Stars wanaume na wanawake,Kigamboni wanawake,Dodoma Combine Wanaume,Star Girls na nyingine zitachuana kupata Klabu bingwa ya Taifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi