Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Sagini na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge Yafanya Ziara Jamhuri ya Afrika ya Kati
Sep 05, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Meja Asia Hussein

Ni ziara maalum ya Kamati ya kudumu ya Ulinzi na Usalama ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Jumanne Abdallah Sagini.

Mheshimiwa Sagini akimbatana na wajumbe wa kamati hiyo, wamewasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kupokelewa na mwambata Jeshi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa nchini Marekani, Brigedia Generali George Mwita Itang’are na wawakilishi kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Maafisa na Askari mbalimbali wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSCA.

Naibu Waziri Jumanne Sagini amepata wasaa wa kufanya mazungumzo na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya ulinzi wa Amani hapa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Luteni Jenerali Sidik Daniel Traole katika Makao Makuu ya MINUSCA yaliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.

Mazungumzo hayo yamelenga kufahamu utendaji kazi wa vikundi vya walinda amani kutoka Tanzania, mafanikio, changamoto zinazokabilivikundi pamoja na mahitajio ya kuwezesha ufanisi na weledi zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Aidha, Naibu Waziri Jumanne Sagini alifanya mazungumzo na walinda amani wa TANBAT 05 waliopo katika wilaya ya Berberati, Mkoa wa Mambere Kadei kwa njia ya mtandao na kupokea taarifa ya utendaji kazi wa kikosi hicho kinachoongozwa na Luteni Kanali Adamu Hamisi Kiza

Naibu Waziri na ujumbe wake wamepongeza kazi zinazofanywa na walinda amani na kuhimiza kuzingatia na kufuata miiko na maadili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kuzingatia tamaduni za nchi husika na washirika wa umoja wa mataifa na kisha wakasisitiza kwa walinda amani juu ya kudumisha nidhamu ya kijeshi kama walivyopokea pongezi kuhusu weledi na nidhamu njema inayooneshwa na walinda amani wa Tanzania wawapo katika majukumu ya ulinzi wa amani.

Wanajeshi wa Tanzania wamekuwa wakishiriki katika majukumu ya ulinzi wa amani, ambapo ufanisi wa majukumu yao yanawezeshwa na Jeshi pamoja na Serikali kwa ujumla, kutokana na hali hii, JWTZ wameweza kushiriki katika operesheni za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali ikiwemo Kongo DRC, Lebanon, Msumbiji na hapa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi