[caption id="attachment_1822" align="aligncenter" width="750"] Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.[/caption]
Na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, UJENZI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesema kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
Akizungumza leo mkoani Dodoma, mara baada ya kukagua daraja hilo lililopo katika barabara ya Mayamaya-Mela KM 99.35, Naibu Waziri Ngonyani amesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo na barabara za maingilio katika daraja hilo kutarahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi wa mkoa huo na mikoa jirani ya Manyara na Arusha.
[caption id="attachment_1823" align="aligncenter" width="750"]"Daraja hili na barabara zake ni kiungo muhimu kati ya mkoa huu na mikoa ya Manyara na Arusha na pia inaunganisha nchi ya Tanzania, (Cape Town) South Afrika hadi (Cairo) Misri, hivyo kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka hapa kuelekea maeneo mengine", amesema Eng.Ngonyani.
Aidha, Naibu Waziri ameitaka kampuni ya ujenzi ya Chico kuhakikisha inamaliza daraja hilo ifikapo mwezi wa Kumi mwaka huu kama ilivyoandikwa kwenye mkataba ili wananchi kuweza kulitumia.
Kwa upande wake Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Eng. Leornado Licari, amesema kuwa kwa sasa mradi umefika asilimia 87 ambapo hivi karibuni wanatarajia kuweka lami.
[caption id="attachment_1825" align="aligncenter" width="750"]"Nakuhakikishia kumaliza mradi huu kwa wakati kwani kazi zilizobaki kwa sasa hivi ni chache, kwa hiyo hadi kufikia mwezi Septemba tutakuwa tumeshakamilisha kazi zote", amesisitiza Mhandisi Mshauri Licari.
Naibu Waziri Ngonyani yupo katika ziara ya kikazi ya siku moja katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambapo pamoja na ukaguzi wa daraja hilo pia amekagua madaraja mengine matatu likiwemo la Msui, Kingali na Mela pamoja na ujenzi wa barabara ya Mela-Bonga KM 88.8.