Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Kwandikwa Awapongeza Tanroads Kudhibiti Vitendo vya Rushwa.
Nov 02, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_21574" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Tisa la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Kigoma mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo.[/caption]

Na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mheshimiwa Elias Kwandikwa,  amewapongeza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa mikakati wanayotumia kudhibiti vitendo vya rushwa katika vituo vya mizani hapa nchini.

Akifungua Mkutano wa tisa wa Baraza la Wafanyakazi la TANROADS mjini Kigoma, Naibu Waziri Kwandikwa amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha watendaji wake wote wanakuwa waadilifu ili rasilimali chache zitumike kwa manufaa ya wote.

“Hakikisheni kila mtakaye mkamata kwa vitedo vya rushwa anachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi ili kuonyesha kuwa jambo la rushwa tunalichukia na hatulipendi katika Serikali”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Naye Mtendaji Mkuu Wa Wakala huo Mhandisi Patrick Mfugale, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja watumishi 71  wamefukuzwa kazi katika vituo mbalimbali vya mizani hapa nchini kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ameongeza kuwa TANROADS wamejipanga kuhakikisha miradi yote ya ujenzi na vituo vya mizani vinafanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kujenga imani kwa wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Hawa Mmanga, amemuhakikishia Naibu Waziri wa Ujenzi kuwa wakala wake umejipanga kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja hapa nchini kwa wakati, ubora na kuzingatia thamani ya fedha.

Wajumbe wa baraza la TANROADS kutoka mikoa yote  nchini wamekutana katika mkutano wa tisa wa baraza la wafanyakazi ili kutathimini utendaji kazi wao na kuibua mikakati mipya itakayowezesha wakala huo kufanya kazi zake kwa weledi na kwa kukidhi mahitaji ya nchi.

 

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi