Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Kanyasu Apiga Marufuku Ukamataji Mchanga Pori la Akiba Rungwa 
May 07, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_42815" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Pori la Akiba la Rungwa lililopo katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singida mara baada ya kuzungumza nao kuhusu ukamati wa vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa una madini ya dhahabu baadala ya kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo ndani ya Pori hilo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Pori hilo, Patrick Kutondolana.[/caption]

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amepiga marufuku ukamataji wa vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya dhahabu unaochimbwa na wachimbaji wadogo wadogo ndani ya Pori la Akiba la Rungwa wilayani Manyoni, mkoani Singida kinyume cha sheria na kuuagiza Uongozi wa Pori hilo kuhakikisha unaimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayodaiwa kuwa na madini ndani ya pori hilo ili kuzuia Wachimbaji kuingia na kuendesha shughuli ya uchimbaji wa mchanga kinyume cha sheria.

Agizo hilo limekuja kufuatia taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Maafisa Wanyamapori ambao wamekuwa wakiwaruhusu Wachimbaji hao kuingia ndani ya Pori hilo nyakati za usiku kwa ajili ya kuchimba mchanga unaodaiwa kuwa una madini kwa makubaliano yaliyo nje ya utaratibu.

Akizungumza na Watumishi wa geti la Doroto katika Pori hilo wilayani Manyoni mkoani Singida, Mhe.Kanyasu amesema kuwa tuhuma hizo za rushwa zitaisha tu pale watakapoimarisha ulinzi katika eneo hilo na sio kukamata vifurushi vya mchanga kwenye geti hilo.

[caption id="attachment_42816" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya watumishi wa Pori la Akiba la Rungwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kuhusu ukamataji wa mchanga unaodaiwa kuwa na madini ya dhahabu wakati alipofanya ziara katika geti la Doroto katika Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.[/caption]

Ameuagiza Uongozi huo kuhakikisha unakamata vifurushi wanavyohisi ndani yake kuna madini na lazima Afisa Madini awepo ili kuhakikisha anataja thamani ya madini pamoja na taratibu zinazotakiwa kufuatwa ili kukidhi matakwa ya sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa.

Baadhi ya Wachimbaji wadogo walionyang'anywa mchanga wao wamedai kwamba Maafisa hao wamekuwa wakikagua magari kwenye geti la kutokea la Doroto na pale wanapokamata vifurushi hivyo bila kujua mchanga huo una madini kiasi gani wamekuwa wakimruhusu mtuhumiwa aende zake bila kumueleza taratibu zozote zile jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Amesema kitendo hicho ni unyang'anyi na uonevu wa hali ya juu na ni kinyume cha sheria kwa sababu sheria ya utaifishaji wa mali iliyokamatwa inampa nafasi mtuhumiwa kujua thamani ya mali aliyokamatwa nayo  na ndipo taratibu za kesi kwenda mahakamani hufuata.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaonya Maafisa Wanyamapori katika pori hilo kuacha tabia ya kuwaonesha wachimbaji hao mahali wanapohisi kuwa kuna madini kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

[caption id="attachment_42817" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza kuzungumza na baadhi ya Watumishi wa Pori la Akiba la Rungwa lililopo katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida kuhusu ukamati wa vifurushi vya mchanga unaodaiwa kuwa una madini ya dhahabu . Wa kwanza kulia ni Meneja wa Pori hilo,Patrick Kutondolana[/caption]

Amesema ni ngumu kwa Mwananchi yeyote kujua sehemu ambako kuna madini ndani ya Pori bila kudokezwa na wenyeji ambao ni Wahifadhi wa Pori hilo

Amesisitiza kuwa endapo uchimbaji huo wa madini ndani ya Hifadhi utaendelea kufanyika itakuwa ni ushahidi tosha kuwa Meneja wa Pori hilo kashindwa kazi.

Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Pori hilo ili kukomesha ujangili wanyamapori pamoja na ukataji miti ndani ya Pori hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa Pori la Akiba la Rungwa, Patrick Kutondolana amekiri kuwa wamekuwa wakikamata mchanga huo kwa mashirikiano kati ya Kamati ya Ulinzi wa Wilaya hiyo ili kukomesha tabia hiyo ya uchimbaji mchanga ndani ya Hifadhi.

Amesisitiza kuwa si kweli kuwa wamekuwa na ushirikiano na Wachimbaji hao kwa makubaliano ya kupata rushwa ni kwamba hiyo imekuwa njama ya kutaka kuwachafua kwa lengo la kuwakatisha nia.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi