Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Japhet Hasunga Afanya Kikao na Wenyeviti wa Bodi Pamoja na Wakuu wa Taasisi Zilizo Chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii Jijini Arusha
Oct 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36368" align="aligncenter" width="800"] 1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kulia) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii wakati akifungua kikao cha kutathimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu kilichofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki.[/caption] [caption id="attachment_36369" align="aligncenter" width="800"] 2. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ( wa pili kulia) akifungua kikao cha Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii kwa ajili ya kutathimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu. Wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Prof. Abiud Kaswamila pamoja na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANAPA.[/caption] [caption id="attachment_36370" align="aligncenter" width="800"] 3. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga ( katikati) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania, Allan Kijazi wakati alipokuwa akiwasili kwa ajili ya kikao na Wenyeviti wa Bodi pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii kilichofanyika jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_36371" align="aligncenter" width="800"] 4. Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani ( wa kwanza)ambaye pia ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi za Taifa akizungumzia hatua za kuchukua katika uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu,[/caption] [caption id="attachment_36372" align="aligncenter" width="800"] 5. Mjumbe wa Sekretarieti wa hatua za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Maliasili na Utalii, Meinrad Rweyemamu akitoa ufafanuzi wa kisheria kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga jana kwenye kikao kwa Wenyeviti na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kilichofanyika jijini Arusha.[/caption] [caption id="attachment_36373" align="aligncenter" width="800"] 6. Naibu Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii( wa kwanza kushoto) akizungumza na Wenyeviti wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii kwenye kikao cha kutahimini hatua zilizofikiwa katika ukamilishaji wa taratibu za uanzishwaji rasmi wa Jeshi Usu. Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga.(Picha Zote na Lusungu Helela)[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi