Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Hasunga Aonya Ukataji Miti Hovyo Mkoani Songwe
Oct 19, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_37036" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akimsikiliza huku akiwa anaandika swali analoulizwa na zungumza Ester Mwakanja kuhusiana athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.[/caption]

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amewaonya watu wenye tabia ya kukata miti hovyo kuwa Serikali haitosita kuwachukulia hatua za kisheria kutokana na kushamiri kwa uharibifu wa misitu mkoani Songwe.

Ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika Mkoa wa Songwe.

Amesema kufuatia kasi ya ukataji miti ovyo inayoendelea  kwa ajili ya mbao na nishati ya mkaa katika maeneo hayo kunatishia kutoweka kwa mvua wanayoitegemea kwa ajili ya kilimo cha mazao ya kahawa, mahindi pamoja na mazao mengine.

Amewaeleza Wananchi hao  kuwa uharibifu huo ukiendelea utaawathiri wao wenyewe  kwa vile mvua itakoma kunyesha katika maeneo yao.

[caption id="attachment_37037" align="aligncenter" width="800"] Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akisoma karatasi katika mkutano wa hadhara ulioufanya katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe[/caption]

Amewataka wakikata mti wapande miti na wale wanaokata miti kwa ajili ya nishati ya mkaa wafuate kanuni na sheria ili kuepuka kukabiliana na Wakala wa Huduma za Misitu  Tanzania (TFS)

Aidha, Mhe. Hasunga Amewataka Wananchi hao kuwa  hata pale inapotokea wanataka kukata mti wa mwembe uliopo katika nyumba zao wanatakiwa kuomba kibali kutoka TFS.

Pia,  Waziri Hasunga amewaagiza TFS itoe miche 10,000 kwa Kata ya Wasa msimu wa mvua utakapokaribia kufuatia ombi la mwanakijji Kasian Mwanjala alilowasilisha kwa Mhe. Hasunga kuwa wanataka kupanda miti ili wanakosa miche.

[caption id="attachment_37038" align="aligncenter" width="800"] Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza jana na wananchi kuhusu athari za ukataji miti ovyo kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isalalo kata ya Wasa wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe.[/caption] [caption id="attachment_37039" align="aligncenter" width="800"] Baadhi ya Watendaji aliokuwa ameongozana nao katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji cha Isalalo.[/caption]

Katika hatua nyingine, Mhe.Hasunga ambaye ni Mbunge katika jimbo la Vwawa lililopo mkoani hapo amewahakikishia wananchi wake kuwa ifikapo mwakani kata ya Wasa itapata umeme wa REA hali itakayosaidia kuboresha maisha kwa wananchi wake.

"Moja ya ahadi yangu niliyoitoa kwenu ni kuhakikisha katika jimbo langu wananchi mnapata umeme, hadi sasa tayari nguzo za umeme zimeanza kuwekwa " amesema Mhe Hasunga.

     

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi