Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Naibu Waziri Angeline Mabula Aipa Kongole NBC
Mar 10, 2020
Na Msemaji Mkuu

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuanzisha utaratibu wa kutembelea viongozi wanawake kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusiana na uboreshaji huduma za benki hiyo.

Dkt. Mabula alitoa pongezi hizo jana ofisini kwake jijini Dodoma baada ya kutembelewa na ujumbe wa NBC ukiiongozwa na Meneja wa Tawi la Benki hiyo jijini humo Bi. Happiness Kizigira ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Alisema, utaratibu ulioanzishwa na Benki ya Taifa ya Bisahara (NBC) kwa kutumia maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kutembelea viongozi wanawake kwenye maeneo tofauti nchini ni mzuri na wa kipekee unaotoa fursa kwa benki hiyo kubadilishana mawazo kupitia viongozi hao kwa lengo la kuboresha huduma zake.

‘’Kwanza nashukuru sana kwa kumfuata mwanamke pale mahali alipo, aina hii inavutia na inatoa muda wa kubadilishana mawazo, iko very unique badala ya kwenda viwanjani. Alisema Dkt Mabula.

Aliueleza ujumbe huo wa NBC tawi la Dodoma kuwa, pamoja na benki hiyo kutumia fursa hiyo kuelezea shughuli zake lakini inatoa nafasi pia kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wateja wake kupitia wanawake kutokana na kuwa na nafasi kubwa kuufikisha ujumbe kwa   wananchi wengi.

Kwa upande wake Meneja wa NBC tawi la Dodoma Bi.Happiness Kizigira alisema, benki yake imeanzisha utaratibu wa kuwatembelea viongozi wanawake kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ili kutoa shukurani sambamba na kuthamini mchango wa wanawake katika shughuli za ujenzi wa taifa.

Kwa mujibu wa Kizigira, wanawake ni jeshi kubwa linalohitaji kuungwa mkono ndiyo maana benki yake imeamua kuwatumia kufikisha ujumbe wa namna bora ya kutunza fedha kupitia Benki ya Taifa ya Biashara.

Meneja huyo wa NBC tawi la Dodoma aliongeza kuwa, benki yake inahamasisha wanawake kutunza fedha kupitia benki hiyo ili kujikwamua kiuchumi na kubainisha kuwa kwa sasa NBC ina huduma nyingi ikiwemo mikopo ya riba nafuu sambamba na ufunguaji akaunti wa haraka unaojulikana kama ‘Faster Acc’ alioueleza kuwa unamuwezesha mteja kufungua akaunti ndani ya muda mfupi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi