Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwongozo wa Tathmini ya Mazingira Kuchochea Ukuaji wa Uchumi
May 18, 2018
Na Msemaji Mkuu

Frank Mvungi

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amezindua Mwongozo wa Tathmini ya Mazingira  (SEA) ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kulinda mazingira ili yaweze kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta  maendeleo  endelevu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo  Jijini Dodoma Waziri Makamba amesema kuwa dhamira ya Serikli ni kuhakikisha kuwa miradi yote mikubwa inayotekelezwa na Serikali pamoja na wawekezaji inafanyiwa tathmini hiyo ili kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.

"Nawapongeza WWF kwa kazi nzuri za tafiti wanazofanya na hata kupatikana kwa muongozo huu ni matokeo ya kazi nzuri waliyofanya kama wadau wetu ambao wamekuwa wanashiriki kikamilifu kuunga mkono juhudi za Serikali kulinda mazingira " Alisisitiza  Mhe. Makamba

Akifafanua amesema kuwa anazikumbusha Wizara ,  Taasisi na wadau wote wanaotaka kutekeleza  miradi ya maendeelo kuhakikisha kuwa wanazingatia muongozo huo ambao umekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inajenga uchumi wa viwanda.

Aliongeza kuwa Ofisi yake ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa SEA  katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo alibainisha kuwa ripoti 14 zimeshapata kibali cha Tathmini ya athari za mazingira na kuongeza kuwa changamoto ambayo Serikali  inachukua kwa uzito kwa sasa ni upatikanaji wa Maafisa Mazingira katika Halmashauri zote hapa nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa  kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,  Biashara na Mazingira Mhe. Sadiq Morad amesema kuwa ili Taifa lifanikiwe katika ujenzi wa uchumi wa viwanda unaotegemea zaidi hifadhi ya mazingira hivyo kuwepo kwa mwongozo huo ni jambo la kimapinduzi katika sekta ya mazingira.

Aliongeza kuwa Kamati hiyo imeridhishwa na hatua hiyo kwani itasaidia katika kuchochea maendeleo na kukuza uchumi kwa maslahi ya Taifa.

Uzinduzi wa Mwongozo huo umefanyika  Jijini Dodoma  na utakuwa chachu ya utunzaji  wa mazingira hapa nchini .

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi