[caption id="attachment_2500" align="aligncenter" width="735"] Picha ya Marehemu Francis Maige Kanyasu maarufu kwa jina la Mzee Ngosha anayesaidikiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa ikiwa katika eneo maalum la kuagia miili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa zoezi la kuuaga mwili wake leo Jijini Dar es Salaam. Mwili huo umeagwa leo na kuelekea Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya mazishi ambapo Serikali inawakilisha na Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii – Wazee na Walemavu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi. Beatrice Fungamo.[/caption]
[caption id="attachment_2501" align="aligncenter" width="750"]
Mwenyekiti wa Mtaa wa Malapa,Buguruni Jijini Dar es Salaam Karim Mahamoud Malapa akisaini kibali cha mazishi ya Mzee Francis Maige Kanyasu nayesadikia kuwa mmoja wa wabunifu wa nembo ya Taifa wakati wa hafla ya kuaga mwili wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mfanyakazi wa Hospitali hiyo Mganga Muya. Mzee Ngosha alipokelewa katika Hospitali hiyo mnamo tarehe 25 nakufanyiwa vipimo na kubainika na maradhi ya Kifua na kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkuta majira ya saa 2:30 usiku wa tarehe 29 2017.[/caption]
Na: Frank Shija
Wasanii nchini watakiwa kufuata taratibu na kujiunga katika vyama vyao ili kujiweka katika mazingira rafiki ya utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kusaidiana katika kutatua changamoto zinazowakabili.
[caption id="attachment_2503" align="aligncenter" width="750"]Wito huo umetolewa leo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mungereza ambaye alimwakilisha Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika zoezi la kuaga mwili wa anayedaiwa kuwa mbunifu wa Nembo ya Taifa, Mzee Francis Maige Kanyasu zoezi lililofanyka Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam leo.
Mungereza alisema kuwa utaratibu wa kuwepo kwa vyama vya wasanii ni wa ,uda mrefu tangu miaka ya sitini ambapo wasanii wamekuwa wakijiunga katika vyama hivyo kwa leong la kuwa na sauti ya pamoja.
[caption id="attachment_2506" align="aligncenter" width="750"]“Mhe. Waziri anasema wazee wa namna hii,na wasanii kwa ujumla ni vizuri tukafuata taratibu kwa mujibu wa sheria, hii itasaidia wasanii kutambulika,kujitangaza na kufahamiana,” alisema Mungereza.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga alisema kuwa Mzee Ngosha amefariki kutokana na maradhi makubwa ya Kifua Kikuu kilichotokana na kuugua kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu.
[caption id="attachment_2508" align="aligncenter" width="750"]Aidha Dkt. Mfinanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi kujenga utamaduni wa kuwahi kufika katika vituo vya tiba punde wanapohisi kuwa na matatizo ya kiafya kwani kufanya hivyo watakuwa wamejiweka katika mazingira mazuri ya kuepuka vifo visivyotarajiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Malapa, Buguruni ameipongeza Serikali kwa jitihada ilizofanya za kuhakikisha inawapata ndugu zake jambo lililopelekea mzee Francis Kanyasu kusafirishwa na kwenda kuzikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Igokero Misungwi Mkoani Mwanza.
Marehemu Mzee Francis Maige Kanyasu maarufu Ngosha alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili mnamo tarehe 25 Mei akitokea katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kufuatia jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo alifanyiwa vipimo na matibabu hadi mauti yalipomkuta majira ya saa 2:30 usiku siku ya tarehe 29, Mei, 2017.Mzee Ngosha anadiawa kuwa miongoni mwa wabunifu wa Nembo ya Taifa jambo ambalo amekufa kukiwa hakuna uhakika juu ya suala hilo.