Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwijage awataka Wahandisi Kujiongeza
Jun 27, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_33105" align="aligncenter" width="750"] Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.[/caption]  

Na Jacquiline Mrisho.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka wahandisi nchini kujiongeza katika kutafuta fursa mbalimbali zikiwemo za ujasiriamali ili kujiongezea kipato.

Mwijage ameyazungumza hayo leo jijini Dodoma wakati akizindua Kongamano la Wahandisi zaidi ya 300 lililohusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).

[caption id="attachment_33106" align="aligncenter" width="750"]  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema akitoa neno fupi la kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (hayupo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.[/caption]

Waziri Mwijage amesema kuwa hakuna mtu anaezuiliwa kufanya kazi nyingine tofauti na aliyosomea hivyo hata Wahandisi wanaweza kufanya ujasiriamali wa aina yoyote.

”Nawaomba Wahandisi kuchangamkia fursa pindi zinapotokea, mjitahidi mpate elimu ya ujasiriamali kwani Serikali itawatumia hata mkiwa katika Taasisi Binafsi", alisema Mwijage.

Aidha, Waziri Mwijage ametoa rai kwa Wahandisi kuungana kufanya kazi kwa pamoja bila ubaguzi ili kuwa pamoja katika ujenzi wa viwanda utakaopelekea nchi kuwa na uchumi wa kati.

[caption id="attachment_33107" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Patrick Barozi akizungumza na Wahandisi (hawapo pichani) wakati wa Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.[/caption] [caption id="attachment_33108" align="aligncenter" width="750"] Baadhi ya Wahandisi walioshiriki katika Kongamano la Wahandisi kuhusu ushiriki wao katika maendeleo ya ujenzi wa viwanda kuelekea katika Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB). Kongamano hilo limefanyika leo jijini Dodoma.[/caption]

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, Mhandisi Prof. Ninatubu Lema amesema kuwa moja ya majukumu ya ERB ni kuhamasisha shughuli za uhandisi hasa katika shule na Vyuo Vikuu mbalimbali ili kwa miaka ijayo nchi ipate Wahandisi wengi watakaojenga miundombinu mbalimbali.

”Hadi kufikia leo, ERB imesajili jumla ya Wahandisi 21,746, tunatoa rai kwa Serikali kuendelea kutuamini kwa kutoa fursa zaidi kwa Wahandisi wa ndani kujenga miradi ya ujenzi inayoanzishwa nchini,” alisema Prof. Lema.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi imeanzishwa kisheria mnamo Oktoba 10, 1968 kwa lengo la kusajili na kusimamia aina zote za Wahandisi na kukuza maendeleo ya uwezo wao kwa lengo la kulinda watumiaji wa huduma za ujenzi nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi