Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwanri: Halmashauri Zinapaswa Kuibua Viwanda 12 kwa Mwaka.
Nov 21, 2017
Na Msemaji Mkuu

Na Tiganya Vincent - RS , Tabora

SERIKALI ya Mkoa wa Tabora izimetaka Halmashauri zote kuanza mara moja utekelezaji wa agizo la ujenzi  na uibuaji wa viwanda visivyopungua 12 katika kipindi mwaka mmoja kuanzia mwezi ujao katika maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Alisema kuwa ni vema kila Mkurugenzi Mtendaji anapaswa kukahikisha kuwa anaanza mara moja utekelezaji wa agizo hilo la ujenzi wa viwanda ili ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao kila eneo liwe na viwanda vipya.

Mwanri alisisitiza kuwa wanatakiwa kuhakikisha kuwepo na viwanda vipya vidogo na vya kati kulingana na maagizo ya viongozi.

Alisema kuwa hatua itawezesha kusaidia vijana wengi kupata ajira au kujiari katika viwanda hivyo vitakavyoanzisha na kuwezesha kufikia nchi ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda.

Mwanri alisema katika kufanikisha dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda, Maafsia Ugani wote katika kipindi hiki cha msimu wa mvua watakiwa kwenda vijijini kuwasaidia wakulima ili wawaze kuzalisha malighafi nyingi za kilimo.

Alisema kuwa Mkoa wa Tabora unaendelea kusisitiza kilimo cha mazao kama vile alizeti, mihogo, mpunga, korosho, maembe, karanga kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwandani. Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kaliua Revocatus Kuuli alisema tayari wataalamu wake wameshaanza kubainisha viwanda vipya ambavyo wataanzisha katika eneo hilo.

Alisema kuwa kwa upande wao wanatarajia kuvuka lengo na kuwa na viwanda vingi ambavyo vitasaidia kutoa ajira kwa vijana wa eneo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi