Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwanjelwa Ataka Huduma za TEHAMA Zifike Vijijini kwa Wananchi
Feb 01, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40002" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa akifungua kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma[/caption]  

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa ametaka huduma za TEHAMA zifike kwa wananchi wa vijijini.

Dkt. Mwanjelwa ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Pili cha Serikali Mtandao cha mwaka 2019 kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma mkoani humo kwa viongozi waandamizi wa Serikali ikiwemo Makatibu Wakuu, wakuu wa Taasisi, mashirika na Idara mbali mbali za Serikali, wataalamu wa TEHAMA na watumishi wengine wa umma

“Tunaelewa wananchi wengi wanaishi vijijini, hivyo tuhakikishe huduma za TEHAMA na za serikali mtandao zinafika kwa wananchi kwa haraka na tuhakikishe tuna wataalamu wa kutosha wa TEHAMA na wa serikali mtandao,” amesema Dkt. Mwanjelwa.

Pia, ameongeza kuwa taasisi zote za umma zizingatie usalama mtandaoni katika hatua zote za kujenga na kutumia mifumo mbali mbali ya TEHAMA na zishirikiane na Wakala wa Serikali Mtandao katika kubuni na kutumia TEHAMA na matumizi ya serikali mtandao. Ameongeza kuwa utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao utakuwa ni kichocheo cha maendeleo ya TEHAMA nchini kwa kuwa itawezesha utoaji wa taarifa ufanyike kwa wakati na kwa haraka

[caption id="attachment_40003" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa (mwenye kilemba) akimsikiliza mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Nguse Ngulumbi kuhusu mfumo wa matumizi ya pamoja ya miundombinu ya TEHAMA ya kutunza taarifa. Wa kwanza kushoto na kulia kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari[/caption]

“Taasisi za umma zishirikiane na Wakala wa Serikali Mtandao kwenye hatua za awali za manunuzi ya vifaa, huduma na mifumo ya TEHAMA nchini ili taasisi husika iweze kupata huduma au vifaa stahiki kutoka kwa mzabuni husika badala ya kuita Wakala wa Serikali Mtandao wakati mambo yameharibika,” amesisitiza Dkt. Mwanjelwa

Dk. Mwanjelwa amesema kuwa huduma za serikali mtandao zitumike kupunguza gharama za utoaji huduma ili kuboresha huduma za Serikali kwa wananchi wake ili kuweza kuendana na kauli mbiu ya kikao hicho isemayo, “Uwianishaji wa Rasilimali za TEHAMA kwa Maendeleo ya Viwanda,” kwa kuwa TEHAMA ni mtambuka na inatumika kwenye sekta nyingine za kiuchumi na kijamii

Aidha, amesema kuwa Serikali imeweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kuwa TEHAMA inatumika kuwahudumia wananchi na watumie kikao hicho kuhakikisha kuwa utoaji wa huduma za Serikali kwa kutumia TEHAMA unakuwa na tija zaidi ili Serikali ifikie azma yake ya kuwahudumia wananchi

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki, amesema kuwa Serikali imejenga miundombinu ya TEHAMA ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, kuhuisha Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003 na kuwa na Sera mpya ya mwaka 2016 inayokwenda na wakati sambamba na mabadiliko ya TEHAMA na ukuaji wake nchini.

[caption id="attachment_40004" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge kabla ya ufunguzi wa kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma[/caption]  

Dkt. Sasabo ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara yake imetunga sheria, kanuni na taratibu mbali mbali zinazosimamia na kuendesha Sekta ya Mawasiliano nchini ambapo imewezesha Serikali kujenga miundombinu ya TEHAMA na kutoa huduma za serikali mtandao ndani ya Serikali na kwa wananchi kwa ujumla ikiwemo pamoja na mifumo mbali mbali ya TEHAMA iliyowekwa na Serikali kama vile mifumo ya malipo, afya, watumishi na utoaji taarifa mbali mbali.

Akiwakaribisha viongozi na wataalamu hao kwenye kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilithi Mahenge amewataka washiriki wa kikao hicho kwenda kutumia huduma za serikali mtandao kwa vitendo ili kuongeza ubora wa utoaji wa huduma za Serikali

“Sasa hivi watu wana nunua simu janja za kisasa ila matumizi yake ni machache wakati tungetumia vizuri zaidi zingebadilisha mwenendo wa maisha yetu,” amesema Dkt. Mahenge.

Kikao hicho cha Pili kimehudhuriwa na jumla ya watu 753 kikifuatiwa na kikao cha kwanza kilichofanyika Arusha, mwezi Oktoba mwaka 2015. Lengo la kikao hicho ni kuwakutanisha viongozi na wataalamu wa TEHAMA ili kubadilishana uzoefu, kujadiliana, kupanga mikakati ya namna ya kutatua changamoto mbali mbali zilizopo kwenye Sekta ya TEHAMA na matumizi ya serikali mtandao ili kuweza kuongeza ufanisi na kuleta tija katika kuwahudumia wananchi

[caption id="attachment_40005" align="aligncenter" width="750"] Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Mary Mwanjelwa (aliyeketi katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na waandaji wa kikao Kazi cha Pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dodoma, Dodoma. Wa kwanza kushoto aliyekaa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Suzan Mlawi[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi