Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Wananchi Tembeleeni Maonesho Kujua Elimu Ya Lishe Bora-Rc Singida
Oct 12, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_48026" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu toka Wizara ya Kilimo, Bw. Mbaraka K. Omar alipowasili katika viwanja vya Bombadier mjini Singida leo kwa ajili ya kutembelea mabanda ya Maonesho ya kuadhimisha Siku ya Chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyikia katika viwanja hivyo. Kauli mbiuya maadhimisho hayo ni; Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa. Maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13 Oktoba, 2019.[/caption]

Na: Kitengo cha Mawasiliano Serikali Wizara ya Kilimo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi leo Ijumaa ametembelea mabanda ya maonesho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani  yanayofanyika Kitaifa katika uwanja wa Bombardier,Manispaa ya Singida.

Amesema uwepo wa maadhimisho haya ni fursa kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa lishe bora kwa afya . [caption id="attachment_48027" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe kwa ajili ya kutembelea mabanda ya Maonesho ya kuadhimisha Siku ya Chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyikia katika viwanja hivyo. Kauli mbiuya maadhimisho hayo ni; Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa. Maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13 Oktoba, 2019.[/caption] [caption id="attachment_48028" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Revocatus Kasimba akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Singida aliyetembelea mabanda ya washiriki wa maonesho ya bidhaa ya chakula na lishe ikiwa ni maadhimisho ya siku ya chakula dunia leo mjini Singida. Maadhimsho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Singidayakiwa na kauli mbiu ya Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa. Maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13 Oktoba, 2019.[/caption]

Amebainisha kuwa elimu juu ya uandaaji chakula tangu kikiwa shambani,baada ya mavuno,wakati wa kukiandaa nyumbani na wakati wa kupika inatakiwa ili mwananchi ale mlo kamili na bora.

Mhe.Dkt.Nchimbi amewasihi wataalam wa lishe nchini kutoa elimu sahihi kwa wananchi kuelewa makundi  muhimu ya chakula kinachopaswa kutumiwa na binadamu. [caption id="attachment_48029" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akipima uzito alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo mkoani humo katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe kwa ajili Maonesho ya kuadhimisha Siku ya Chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyikia katika viwanja vya Bombadier mkoani humo. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa. Maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13 Oktoba, 2019.[/caption] [caption id="attachment_48030" align="aligncenter" width="1000"] Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akipokea matokea ya vipomo vyake mara baada ya kufanya tathmini ya lishe kwa kupima uwiano wa urefu na uzito uzito alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo mkoani humo katika maonesho ya bidhaa za chakula na lishe kwa ajili Maonesho ya kuadhimisha Siku ya Chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyikia katika viwanja vya Bombadier mkoani humo. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni; Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa. Maadhimisho hayo yatazinduliwa rasmi tarehe 13 Oktoba, 2019.[/caption]

"Uwepo wa maadhimisho haya ya kitaifa Singida usaidie jamii kutambua umuhimu wa lishe bora kwa ustawi wa afya za watu ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa"Mhe. Nchimbi

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kupata elimu juu ya lishe bora na teknolojia rahisi ya kuongeza thamani ya mazao ya chakula.

Uzinduzi rasmi wa maadhimisho hayo utafanyika Jumapili ijayo na yatahitimishwa tarehe 16 mwezi huu.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni " Lishe Bora kwa Ulimwengu Usio na Njaa".

I  

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi