Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwakyembe Aipongeza TBC kwa Kuongeza Usikivu Mipakani mwa Tanzani
Feb 04, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_28476" align="aligncenter" width="1000"] Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe akiwapongeza viongozi na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa kuongeza usikivu kwa maeneo ya mipakani (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayoub Rioba (Picha na Anitha Jonas).[/caption]

Na. Anitha Jonas – WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ameupongeza uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuongeza usikivu katika maeneo mbalimbali ya mipakani mwa nchi.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi hizo alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo katika mkutano huo walijadili mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya bajeti na mwenendo wa shirika hilo.

Dkt. Mwakyembe alisema: “Ninafuraha kubwa kupata taarifa ya  kuimarika kwa usikivu katika maeneo ya mipakani yaliyokuwa na yanasumbua kwa muda mrefu kama maeneo ya Tarakea, Kibondo, Longido,Tarime na Mbambabay pamoja na maeneo ya Mtwara na Nachingwea,” Dkt.Mwakyembe.

[caption id="attachment_28477" align="aligncenter" width="1000"] Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba akitoa taarifa ya upanuzi wa usikivu wa matangazo ya Shirika hilo nchini kwa Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (Kushoto) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliyofanyika jana jijini Dar es Salaam (Picha na Anitha Jonas).[/caption]

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Waziri Mwakyembe aliupongeza uongozi wa TBC kwa kufanya maamuzi ya kutumia mafundi mitambo wa ofisi yao kwa ajili ya kufunga mitambo hiyo pamoja na kufanya matengenezo pia aliwapongeza mafundi mitambo waliofanya kazi hiyo kwa uaminifu na uzalendo huku akiomba uongozi wa shirika hilo kuwatambulisha bungeni mafundi hao wakati wa bunge la bajeti.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt. Ayoub Rioba alieleza kuwa mpaka sasa  katika Wilaya ya Geita, tayari Shirika limefunga mitambo mipya inayosaidia  kuboresha usikivu wa uhakika na kazi hiyo imefanywa na mafundi wazalendo wa shirika hilo.

Naye  Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Ufundi kutoka TBC Bw. Joseph Kambanga alieleza kuwa mpaka sasa kazi ya kububoresha usikivu inaendelea na baadhi ya mafundi walikuwa Tarime wakiendelea na kazi hiyo na kwa mwezi ujao wanategemea kuongeza usikivu kwa  Mkoa wa Mtwara na Nachingwea.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi