Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mwakalinga Ateta na Watumishi wa Taasisi za Sekta ya Ujenzi
Sep 01, 2020
Na Msemaji Mkuu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Shinyanga Daniel Ojwando, wakati Katibu Mkuu huyo alipokuwa akikagua Karakana ya TEMESA mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi, akizungumza wa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi, wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, alipokutana na watumishi hao mkoani Shinyanga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo kwa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta yake (hawapo pichani) alipokutana nao mkoani Shinyanga kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Ujenzi, wakimsikilizaKatibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga (hayupo pichani) wakati alipokutana nao kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Mfanyakazi kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Shinyanga, Gerryson Lwiza, akitoa maoni yake wakatiKatibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga,  alipokutana na watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta yake kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta hiyo, mkoani Shinyanga, mara baada ya kukutana nao kujadili masuala mbalimbali ya kiutumishi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi