Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Muhimbili Yatumia Muarobaini Huu Kupambana na Msongamano wa Watu, Magari
Aug 10, 2023
Muhimbili Yatumia Muarobaini Huu Kupambana na Msongamano  wa Watu, Magari
Muonekano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Na Ahmed Sagaff

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umechukua hatua mbalimbali kupambana na msongamano wa watu na magari uliobainika baada ya kufanyika utafiti hospitalini hapo.

Akizungumza leo katika Ukumbi wa Idara ya Huduma za Habari jijini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema utafiti ulibaini kwamba kwa siku moja eneo hilo wanaingia watu 20,000 na magari 3,500.

“Hali hii ilitulazimu kuanzisha utaratibu wa kulipia huduma ya maegesho ili isaidie kupunguza msongamano wa magari ndani ya Hospitali.

“Jitihada za kupunguza msongomano Upanga ziligusa pia kuhamisha huduma tatu kwenda Mloganzila kwa lengo lile lile la kupunguza msongamano mkubwa uliokuwepo MNH Upanga. 
“Hali kadhalika tulipunguza idadi ya ndugu wanaokuja kusalimia wagonjwa waliolazwa kutoka watano kwa wakati mmoja hadi wawili asubuhi, mmoja mchana na wawili jioni.

“Utaratibu huu unalinda watumiaji wa huduma wakiwemo wagonjwa na wageni wote wanaoingia na kutoka ndani ya Hospitali,” ameeleza Prof. Janabi.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi