Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Muhimbili Yakusanya Bilioni Mbili Kila Mwezi
Aug 10, 2023
Muhimbili Yakusanya Bilioni Mbili Kila Mwezi
Muonekano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
Na Ahmed Sagaff

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inakusanya mapato ya takriban Shilingi bilioni mbili kila mwezi kutoka kwa wananchi wanaotoa fedha zao kulipia huduma mbalimbali hospitalini hapo.

Akizungumza leo katika Ukumbi wa Idara ya Huduma za Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema mapato hayo yameongezeka kutoka shilingi milioni 900 kwa mwezi.

Aidha, Prof. Janabi ameeleza kuwa fedha hizo zimeusaidia uongozi wa hospitali hiyo kutumia Shilingi bilioni 14 kuwalipa posho na marupurupu wafanyakazi wake, jambo litakalowafanya watekeleze majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Pia, Prof. Janabi amearifu kwamba, hospitalini hapo huwasili wagonjwa 6,200 kila siku kwa ajili ya kufuata matibabu huku wanafunzi 2,000 kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wakiwasili kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.

Vilevile, mtaalamu huyo amebainisha kwamba hospitali hiyo hutoa huduma kwa muda wa masaa 24 kwa siku ili kumsaidia mwananchi kupata huduma za afya muda wote.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi