Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mtambo wa Cathlab wa JKCI Watibu wagonjwa 1004 kwa miezi 11
Dec 12, 2018
Na Msemaji Mkuu

Na Mwandishi  Maalum – Dar es Salaam

Jumla ya wagonjwa 1004 wamefanyiwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kupitia tundu dogo linalotobolewa katika mshipa mkubwa wa damu uliopo kwenye  paja kwa kipindi cha miezi 11na siku 11 .

Upasuaji huo umefanyika kupitia mtambo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi wa matatizo ya moyo na tiba mbalimbali za magonjwa ya moyo uliopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Akiongea na waandishi wa habari leo jiji Dar es Salaam Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya tiba ya moyo alisema hii ni mara ya kwanza kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi kiasi hicho tangu kuanza kufanya kazi kwa mtambo huo mwaka 2013 .

“Mwaka jana kupitia mtambo wa Cathlab tulifanya upasuaji kwa wagonjwa 800 kati ya hao watu wazima walikuwa 708 na watoto 92. Kwa mwaka huu  ambao bado haujamalizia tumetoa tiba kwa wagonjwa  1000 kama wagonjwa hawa 1000 wangeenda kutibia nje ya nchi Serikali ingetumia zaidi ya shilingi bilioni sita”.

“Haya ni mafanikio makubwa yanayotupa motisha na nguvu ya kufanya kazi zaidi ya kuwahudumia wananchi tumejipanga kwa mwaka 2019 kuwaona wagonjwa 1500 kupitia mtambo huu wa Cathlab”, alisema Dkt. Kisenge

Alisema kati wa wagonjwa 1000 waliotibiwa katika mtambo huo  asilimia 70 ni watu wazima na asilimia 30 ni watoto na kuahidi kuendelea  kutoa huduma bora za matibabu ya moyo  zenye uwezo na kiwango cha juu cha kimataifa kwa kuwahudumia na kuwajali wagonjwa wanaofika katika Taasisi hiyo.

Uchunguzi unaofanyika katika mtambo wa Cathlab ni kuangalia  hali ya mishipa ya moyo kwa kuainisha kiwango cha kuziba kwa mishipa hiyo, kuchunguza uwezekano wa mgonjwa kustahili  kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo na kama upasuaji huo utaweza kumsaidia au hautamsaidia mgonjwa na kuchunguza hali ya utendaji kazi wa vifaa bandia vilivyowekwa ndani ya moyo hususani valvu.

Tiba inayotolewa kupitia mtambo huo ni kuzibua mishipa ya moyo iliyoziba, kupandikiza vifaa saidizi vya moyo vinavyosaidia kuongeza mapigo ya moyo ya mgonjwa yaliyo chini, kupandikiza vifaa maalum vinavyoratibu mapigo ya moyo wenye shida na kutoa tiba inapostahili, kutanua valvu za moyo zilizobana, kuzibua matundu kwenye kuta za moyo na kufanya upasuaji ambatano kwa kuhusisha upasuaji wa kufungua kifua unaoambatana na upandikizaji vifaa kwenye moyo.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi