Na Jonas Kamaleki - Msomera
Mkazi wa Msomera aliyehamia hivi karibuni kutoka Ngorongoro amewadhihirishia Makatibu Wakuu na wananchi kuwa Kijiji hicho ni fursa kubwa ya Kiuchumi.
Bwana Samuel Mollel ameanza kilimo kisasa cha mbogamboga cha kutumia umwagiliaji kwa njia ya matone ili kuuza kwa wakazi wa kijiji hicho.
"Ndugu zangu Serikali imetupatia fursa kubwa ambayo si rahisi kujirudia, mimi nimefungua duka kubwa, ninakamilisha ufungaji wa mashine ya kusaga na kukoboa, pia ninaanzisha bekari ya kutengeneza mikate. Jengo la bekari nimeshakamilisha", allisema Mollel.
Mkazi huyo amesema atafuga kwa njia ya kisasa ng'ombe wa maziwa ambao watampatia maziwa ya kuuza na kutosheleza kwa ajili ya mgahawa wake.
Amewataka ambao walikuwa wanapotoshwa kuwa Msomera hakukaliki waupuuze upotoshaji huo wafanye haraka kujiandikisha kwa maana bahati haiji mara mbili.
Bwana Mollel eneo la makazi yake lote amelizungushia uzio ili mifugo ya majirani isijekuharibu mazao yake.