Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mradi wa PS3 Kuimarisha Uandaaji Bajeti
Aug 07, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_8608" align="aligncenter" width="750"] Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari alipokuwa akifungua mafunzo ya Mfumo ulioboreshwa wa kuandaa Mpango wa Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ujulikanao kama ‘planRep’. Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Mkoani Morogoro.

[/caption] [caption id="attachment_8606" align="aligncenter" width="750"] Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA – TAMISEMI, Baltazar Kibola akizungumza na wadau wa Mfumo ulioboreshwa wa kuandaa Mpango wa Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ujulikanao kama ‘planRep’ wakati wa mafunzo ya mfumo huo yaliyofunguliwa leo mkoani Morogoro.[/caption]

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Morogoro.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari amesema kuwa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) umetegemewa kuimarisha utendaji kazi wa Halmashauri nchini kwa kuleta mageuzi makubwa katika eneo la uandaaji wa Bajeti na upangaji wa mipango ya Serikali.

Tandali alisema hayo leo Mkoanmi Morogoro wakati akifungua mafunzo ya Mfumo ulioboreshwa wa kuandaa Mpango wa Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ujulikanao kama ‘planRep’.

Tandari amesema kuwa mradi huo utatumika kuanzia ngazi za chini katika muundo wa Serikali ambapo utawezesha kuandaa bajeti na mipango kulingana na vipaumbele vya mahitaji ya wananchi wa eneo husika hivyo mafunzo hayo yataenda kuboresha zoezi la uandaaji wa mipango na bajeti katika Halmashauri zote nchini.

“Mfumo huu mpya unakwenda kutatua changamoto zilizokuwepo katika mfumo wa zamani zikiwemo za uwepo wa matoleo mengi yanayotumwa kwa wakati mmoja, uwepo wa bajeti tofauti kwenye kila ngazi ya utawala kutumia muda na gharama nyingi hadi kumaliza maandalizi hivyo mfumo huu utaleta mageuzi makubwa katika uandaaji wa Bajeti zetu,” alisema Tandari.

[caption id="" align="alignnone" width="750"]  Baadhi ya wadau wa Mfumo ulioboreshwa wa kuandaa Mpango wa Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa ujulikanao kama ‘planRep’ wakisikiliza hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo mkoani Morogoro.[/caption]

Ameongeza kuwa, kwa kuwa mfumo huu umeboreshwa na utakua mmoja kwa sekta zote hivyo Serikali itakua na bajeti na mipango yenye ubora na ufanisi wa hali ya juu hali itakayopelekea urahisi katika utoaji wa taarifa kwa wadau wa ngazi zote Serikalini.

Aidha, Tandari ametoa rai kwa waboreshaji wa mfumo huo kuangalia namna ya kutumia mfumo hata sehemu ambazo kuna changamoto ya upatikanaji wa mtandao pia amewataka watumiaji wa mfumo huo kuyaelewa vema mafunzo hayo na kuwaelekeza wenzao katika ofisi kwani wenyewe wameteuliwa kushiriki kama wawakilishi wa ofisi walizotoka.

Akiwakilisha viongozi wa Mradi huo, Meneja Mifumo ya TEHAMA, Revocatus Mtesigwa amesema kuwa lengo kuu la mradi huo ni kushirikiana na Serikali katika kuboresha matumizi ya rasilimali zilizopo kwa kuboresha usimamizi wa fedha katika ngazi za kutolea huduma zikiwemo za vituo vya kutolea huduma za afya na elimu.

“Mradi huu unafanya kazi katika maeneo matano yakiwemo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wa wananchi, Rasilimali watu, Rasilimali fedha, Mifumo ya TEHAMA pamoja na Tafiti Tendaji hivyo matokeo ya kuimarisha mfumo huu kupitia maeneo haya, tutaiwezesha Serikali kuboresha usimamizi, kuongeza ufanisi pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,” alisema Mtesigwa.

Amefafanua kuwa mfumo huo mpya utapunguza gharama za uandaaji wa mipango na bajeti hivyo kuokoa fedha nyingi za Serikali ambazo zitaelekezwa katika kutekeleza miradi mingine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA – TAMISEMI, Baltazar Kibola amesema mafunzo yanayoendelea katika mikoa ya Morogoro, Mbeya na Kigoma ni ya awamu ya pili ambapo awamu ya kwanza yalifanyika Mtwara na Mwanza, kwa mkoa wa Morogogo mafunzo yamejumuisha maafisa wahusika kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Pwani pamoja na Morogoro yenyewe.

Mafunzo haya ya siku 8 yamefadhiliwa na Shirika la Msaada la Marekani (USAID) chini ya mradi huo wa miaka mitano ulioanza mwaka 2015 hadi 2020 unaohusisha maafisa wa Serikali wanaotimia mfumo huo wa PlanRep wakiwemo Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya, Maafisa TEHAMA, Wachumi, Wahasibu na Maafisa Mipango wa Serikali.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi