Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mradi wa Kukuza Maendeleo ya Utamaduni Wazinduliwa Zanzibar
Oct 26, 2023
Mradi wa Kukuza Maendeleo ya Utamaduni Wazinduliwa Zanzibar
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita Maulid akizungumza wakati akizindua Mradi wa UNESCO - ALWALEED PHILANTHROPIES unaolenga kukuza maendeleo ya kijamii kupitia Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) na ajira zinazohusiana na Utamaduni.
Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Mhe. Tabia Mwita Maulid  amezindua Mradi wa UNESCO - ALWALEED PHILANTHROPIES unaolenga kukuza maendeleo ya kijamii kupitia Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) na ajira zinazohusiana na Utamaduni.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mjini Zanzibar, Oktoba 24, 2023, amesema mradi huo utasaidia kutoa elimu ya kulinda Utamaduni pamoja na Wadau wa Utamaduni kunufaika na bidhaa za Utamaduni.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholas Mkapa amesema mradi huo utanufaisha vijana katika Utengenezaji wa Filamu, Muziki na Sanaa kwa kukuza uchumi na kuwawezesha vijana kupata kipato.

Aidha, Mwakilishi wa UNESCO hapa nchini Dkt. Michael Toto amesema lengo la Mradi huo ni kukuza maendeleo ya jamii ya Tanzania kwa kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi na ajira zinazotokana na utamaduni.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi