Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Moi Yaokoa Bilioni 5 kwa Kupunguza Rufaa za Nje ya Nchi
Nov 20, 2017
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_23073" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na menejimenti ya MOI katika ukumbi wa Mikutano MOI

[/caption] [caption id="attachment_23074" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akimjulia hali Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji Mkubwa wa Mgongo , anayetoa ufafanuzi wa namna upasuaji huo ulivyofanyika ni Dkt Nicephorus Rutabansibwa (Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo) . Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje nchi kufuata matibabu baada ya MOI kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira, miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti

Akizungumza na menejimenti ya MOI Dkt Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.

[caption id="attachment_23075" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damu ya MOI
[/caption] [caption id="attachment_23076" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Maabara Bwana Mbuta Jackson ya namna benki mpya ya damu inavyfanya kazi kwa kushirikiana na damu salama[/caption]

“Mnafanya kazi nzuri sana , jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba muongeze ubunifu zaidi. Hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika pekee bali duniani. Hii ni changamoto kwetu sote kuifikisha hapo”. Dkt Ulisubisya

Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na kusiwepo mgonjwa wa kwenda nje. Pia, amewaelekeza viongozi wa MOI kwa kushirikiana na Wizara mama kutafuta namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri kwa wizara

“Azma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh .Dkt John Pombe Magufuli ni kuhakikisha huduma zote za Afya zinapatikana hapa nchini na vyema sote tukamuunga mkono” Dkt Ulisubisya

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi ameupongeza uongozi wa MOI kwa kuwa na maono ya mbali ya kuifanya MOI kuwa Taasisi bora barani Afrika na duniani

[caption id="attachment_23077" align="aligncenter" width="750"] Menejimenti ya MOI wakifuatilkia hotuba ya katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya katika ukumbi wa Mikutano MOI
[/caption] [caption id="attachment_23078" align="aligncenter" width="750"] Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhamad Kambi wakiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya MOI[/caption]

“Nimefurahi kwamba MOI mna maono ya mbali , mnafikiria kuitoa Taasisi hii hapa ilipo na kuifikisha sehemu ya juu zaidi, dira yenu ni kuwa Taasisi bora Afrika kufikia 2022 fanyeni kazi kwa bidii kufikia lengo hilo .” Prof Muhamad Kambi

Awali akiwasilisha taarifa ya Utendaji, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt Respicious Boniface amesema toka kuanzishwa kwa Taasisi imefanikiwa kuanzisha huduma za kibingwa za Upasuaji wa Nyonga, Magoti, Ubongo, Mgongo, Vibiongo, Usingizi ambazo zimesaidia kupunguza rufaa za nje ya nchi.

“Mh Katibu Mkuu ,baada ya kuanzisha huduma hizi za Kibingwa tumefanikiwa kuokoa shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi, tumepunguza rufaa kwa asilimia  kubwa naomba nikuhakikishie hata hizi asilimia 5% zilizobaki tutashirikiana na Serikali na naamini zitakwisha kabisa” Dkt Respicious Boniface

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi