Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MOI Yaendesha Mafunzo Maalum ya Matibabu ya Mifupa ya Kifundo cha Mguu na Mifupa ya Unyayo.
Aug 09, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45971" align="aligncenter" width="750"] 1. Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya madaktari wa mifupa yanayofanyika kwa siku tatu[/caption] [caption id="attachment_45973" align="aligncenter" width="750"] 2. Mratibu wa mafunzo ya madaktari wa mifupa Dkt Samweli Nungu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya upasuaji wa mifupa ya unyayo na kifundo cha mguu. (Foot and Ankle)[/caption] [caption id="attachment_45974" align="aligncenter" width="750"] 3. Dkt Adraan Van Zyl kutoka nchini Afrika Kusini akitoa mada katika mafunzo maalum ya matibabu na upsauji wa mifupa ya unyayo na kifundo cha mguu.[/caption] [caption id="attachment_45975" align="aligncenter" width="750"]  Washiriki wa mafunzo wakifuatilia mada kwa umakini.[/caption]

Dar es Salaam, 08/08/2019.

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Chuo cha Mafunzo cha Madaktari bingwa wa upasuaji cha nchi za Afrika Mashariki, Kati na kusini (COSECSA) pamoja na chama cha madaktari wa Mifupa cha Afrika kusini imeendesha mafunzo maalum ya matibabu ya mifupa ya kifundo cha Mguu na Mifupa ya unyayo.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface.

Dkt.Boniface amesema MOI imekua ikitoa mafunzo kwa kushirikiana na Taasisi na mashirika mbalimbali ya ndani na ya kimataifa kwa lengo la kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani ya nchi pamoja na nchi nyingine za Afrika ili kuboresha huduma zake na kumaliza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

“Washiriki wa mafunzo haya ni madaktari bingwa wa MOI na hospitali nyingine hapa Tanzania pamoja na wanafunzi wanaobobea kwenye upasuaji wa mifupa, wakufunzi wanatoka Afrika kusini na mafunzo yatahusisha nadharia pamoja na mafunzo kwa vitendo ambapo baadhi ya wagonjwa watafanyiwa upasuaji”. Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface amesema Lengo la Mafunzo haya ni kuwapa wataalamu mbinu mpya za upasuaji wa mifupa hususani mifupa ya kifundo cha mguu pamoja na mifupa ya unyayo kwani teknolojia ya matibabu inabidilika kwa haraka sana.

Kwaupande wake Mratibu wa mafunzo hayo Dkt. Samweli Nungu amesema mafunzo yatasaidia kwani madaktari wa mifupa watapewa mbinu mpya na za kisasa za upasuaji wa mifupa ambazo zitasaidia kuleta matokeo bora kwa wagonjwa wenye matatizo hayo na kuepusha ulemavu.

Imetolewa,

Kitengo cha Uhusiano MOI

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi