[caption id="attachment_36786" align="aligncenter" width="576"] Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Mahakama ya Tanzania na Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka uliofanyika katika hoteli ya Morogoro mkoani Morogoro.[/caption]
Na: Victor Kitauka, Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro
Mahakama ya Tanzania haiwezi kutekeleza Mpango Mkakati wake bila kushirikisha na kushauriana na Wadau wake katika jukumu la utoaji haki kwa wananchi.
Hayo yalisemwa wiki iliyopita na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mh. Dr. Eliezer M. Feleshi alipokuwa akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Mahakama ya Tanzania na Madalali wa Mahakama na Wasambaza Nyaraka mjini Morogoro katika hotel ya Morogoro Hotel.
Mhe. Jaji Kiongozi alisema kuwa Mkutano huo ni muhimu sana kwa Mahakama na kwa Wadau (Madalali wa mahakama na Wasambaza Nyaraka ambao ni maafisa wa Mahakama) waliohudhuria katika Mkutano huo.
[caption id="attachment_36788" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kinachojiri.[/caption]“Mkutano huu ni wa kihistoria kwa sababu ni Mkutano unaofanyika kwa mara ya kwanza na pia umewaleta pamoja Madalali na Wasambaza Nyaraka za Mahakama ambao wamehudhuria mafunzo na kufaulu usaili wa kuomba kazi ya Udalali na Usambazaji Nyaraka,” alieleza Mhe. Jaji Kiongozi.
Akizungumzia mkutano huo, Mhe. Jaji Kiongozi alisema lengo ni kujadili na kutathmini masuala mbalimbali yanayohusiana na kazi/huduma wanazofanya Madalali na Wasambaza Nyaraka kwa wadau wengine wa Mahakama.
Kupitia mkutano huu wanatarajia kuja na maazimio ambayo yatasaidia sana katika kutekeleza majukumu ya Mahakama ambayo lengo kuu ni kuiwezesha mahakama kutoa haki kwa wakati.
pia ni mara ya kwanza tangu wameingia kwenye jukumu hilo kwa muundo na sasa na miongozo wa sasa unaosimamia utendaji wa kazi za madalali na Wasambaza Nyaraka kukutana.
[caption id="attachment_36789" align="aligncenter" width="750"] Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi (aliyeketi wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano huo.[/caption]Mahakama ya Tanzania kupitia mpango mkakati wake wa mwaka 2015/2020 ambao una nguzo tatu, ya kwanza ikiwa ni utawala na uwezeshaji, ya pili ni kuhimili kazi kuu ya utoaji haki na tatu ni kuifanya kazi ya mahakama iaminike na kujenga misingi imara ya kushirikia na na wadau wake, na kupitia nguzo ya tatu ndio sababu ya mkutano huu, kwani mahakama umeona haiwezi kufanya majukumu yake bila kupata ushirikiano wa dhati, mipango ya pamoja na hata kushauriana na wadau wake.
Akielezea umuhimu wa Wadau hao katika utoaji wa haki, Mhe. Jaji alisema kuwa wana jukumu kubwa la kutekeleza na kuwezesha usikilizwaji wa mashauri kwa maana ya usambazaji wa nyaraka lakini kutekeleza ukazaji wa hukumu kwa kufika tamati ya wadaawa na hivyo kuwezesha haki kupatikana kwa wakati.
hivyo kutenda vizuri kwa muhusika mmoja au sehemu moja ndani ya mkondo wa utoaji haki hakuwezi kukafanikiwa kama upande au muhusika mwingine hawezi akashikamana na hilo na ndio sababu mahakama ikaona kujenga uwezo wa madali na Wasambaza Nyaraka ni jambo la msingi katika kutekeleza majukumu yake.
Aidha; Mhe. Jaji Kiongozi aliwakumbusha Wadau hao juu ya umuhimu wa kuanzisha chama chao ili kiweze kuwa kama daraja la mawasiliano na Mahakama na pia katika kuwasilisha mapendekezo ya kuboresha kazi zao, changamoto mbalimbali.
“Vilevile Chama kitasaidia kudhibiti Madalali na Wasambaza Nyaraka wanaokwenda kinyume na miiko ya udalali ili kulinda hadhi na heshima ya madalali na Wasambaza Nyaraka,” alisisitiza. Mhe. Jaji Dkt. Feleshi.
Mkutano huo wa siku mbili (2) uliofikia tamati Oktoba 12, uliudhuliwa pia na Mwakilishi kutoka katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Polisi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wengine ni Wawakilishi kutoka TRA, BRELA, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Manaibu Wasajili wa Mahakama Kuu na Hakimu Mkazi Mfawidhi-Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro.