Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

MKURABITA Yawezesha Wakulima Wilayani Chamwino Kujikwamua Kiuchumi
Feb 21, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_40722" align="aligncenter" width="732"] Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia hati za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo wakati wa ufunguzi wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Membe  Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.[/caption]

Frank Mvungi, Dodoma

Mpango wa Kurasimisha  Rasilimali  na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) umepongezwa kwa kuwawezesha wananchi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa kuwajengea uwezo ili waweze kutumia hati za kimila za kumiliki ardhi  kujiletea maendeleo.

Akizungumza leo Wilayani humo wakati akifungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100  wa Kijiji cha Membe mbunge wa jimbo hilo Mhe. Joel Mwaka amesema kuwa wananchi wanajengewa uwezo  ili waweze kutumia hati hizo kujiletea maendeleo ikiwemo kuzitumia kama dhamana kuchukua mikopo katika Taasisi za fedha kama mabenki.

“ Nawapongeza  Ofisi ya Rais- MKURABITA  kwa kuwezesha mashamba 1145 kupimwa na tayari hatimiliki za kimila 1000 zimeweza kuandaliwa ili kuwawezesha wananchi kuzitumia kujikwamua kiuchumi” Alisisitiza  Mwaka.

[caption id="attachment_40719" align="aligncenter" width="900"] Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mhe. Joel Mwaka akifungua mafunzo kwa wakulima waliorasimisha mashamba yao na kupata hati za kimila za kumiliki ardhi kupitia Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) leo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa  kuna umuhimu wa kuunga mkono juhudi za MKURABITA kwani kati ya vijiji 107 vilivyopo katika halmashauri hiyo  ni viwili tu vimebahatika kupata fursa ya kurasimishiwa ardhi na kujengewa uwezo kupitia mafunzo yanayoendeshwa na mpango huo kwa.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kujitokeza kuchukua hati zao ili wazitumie kujikwanua kiuchumi kwa kuwa zimeshandaliwa na ziko tayari.

“ Faida za hati hizi ni pamoja na kuhakikisha usalama wa milki ya mkulima na kuongeza thamani ya ardhi na pia itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Chamwino na Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Mwaka.

Alibainisha kuwa wakulima hao zaidi ya 100 watakuwa chumvi tosha kwa Wilaya hiyo na kuleta mabadiliko makubwa katika uzalishaji kwenye kilimo na ufugaji na hivyo kuongeza tija na kipato kwa wakulima wilayani humo.

[caption id="attachment_40721" align="aligncenter" width="900"] Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Joel Mwaka akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya wananchi walipatiwa hati za kimila za kumiliki ardhi baada ya kurasimisha mashamba yao katika Kijiji cha Membe.[/caption]

Akifafanua amesema kuwa  kuna umuhimu wa kuunga mkono juhudi za MKURABITA kwani kati ya vijiji 107 vilivyopo katika halmashauri hiyo  ni viwili tu vimebahatika kupata fursa ya kurasimishiwa ardhi na kujengewa uwezo kupitia mafunzo yanayoendeshwa na mpango huo kwa.

Aliongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kujitokeza kuchukua hati zao ili wazitumie kujikwanua kiuchumi kwa kuwa zimeshandaliwa na ziko tayari.

“ Faida za hati hizi ni pamoja na kuhakikisha usalama wa milki ya mkulima na kuongeza thamani ya ardhi na pia itasaidia kukuza uchumi wa Wilaya ya Chamwino na Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Mwaka.

Alibainisha kuwa wakulima hao zaidi ya 100 watakuwa chumvi tosha kwa Wilaya hiyo na kuleta mabadiliko makubwa katika uzalishaji kwenye kilimo na ufugaji na hivyo kuongeza tija na kipato kwa wakulima wilayani humo.

[caption id="attachment_40720" align="aligncenter" width="796"] Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Membe Bw. Yoram Majenda leo Wilayani Chamwino mara baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 na viongozi 10 ili wajengewe uwezo wa kutambua fursa zilizopo baada ya kurasimisha mashamba yao na kupata hati milki za kimila za kumiliki ardhi.[/caption]

Kwa upande wake Mratibu wa MKURABITA Bi.  Seraphia Mgembe amesema kuwa Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wanachi wanajikwamua kiuchumi kupitia uwezeshaji unaofanywa kwa kurasimisha mashamba ya wananchi na kuwapa hati ili waweze kuzitumia kujiletea maendeleo.

“ Mkitumia hati hizi vizuri kama Serikali ilivyodhamiria mtajikwamua kichumi kwani hapa kila aliyepewa tayari ajihesabu kuwa yeye ni mmiliki wa ardhi yenye thamani na inayoweza kuleta mageuzi makubwa katika maisha yake” Alisisitiza Bi.  Mghembe

Akifafanua zaidi amesema kuwa ni vyema wananchi wakaepuka vitendo vya kuuza ardhi zao kiholela badala yake wazitumie kwa tija hata pale wanapoamua kuuza sehemu ya maeneo yao walenge kujiletea maendeleo ili kuendana na dhana ya kujenga uchumi jumuishi inayosisistizwa na Serikali .

[caption id="attachment_40718" align="aligncenter" width="862"] Sehemu ya wanachi walioshiriki hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 na viongozi 10 katika kijiji cha Membe wilayani Chamwino mkoani Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Joel Mwaka leo Wilayani humo.[/caption]

MKURABITA itaendesha mafunzo hayo kwa siku tatu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino yakilenga kuwajengea uwezo wakulima wa kijiji cha Membe kuzalisha kwa tija kupitia kilimo cha alizeti, ufugaji na pia watapata kujengewa uwezo kuhusu namna ya kutunza kumbukumbu, utafutaji fursa na namna ya kuzitumia, uandishi wa mpango wa biashara na uundaji wa vikundi vya hiari, utunzaji wa kumbukumbu na uthamini wa ardhi na utunzaji wa mazingira.

[caption id="attachment_40724" align="aligncenter" width="900"] Meneja urasimishaji ardhi vijijini kutoka MKURABITA Bw. Antony Temu akieleza faida za mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima wa Wilaya ya Chamwino katika Kijiji cha Membe ili waweze kutumia hati milki za kimila za kumiliki ardhi walizopata kujiletea maendeleo.[/caption]

(Picha zote na MAELEZO)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi