Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkemia Mkuu wa Serikali Asisitiza Uadilifu kwa Watumishi
Sep 03, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_34765" align="aligncenter" width="750"] Watumishi wapya wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakifuatilia mafunzo elekezi na upekuzi yaliyoanza leo kwenye Ukumbi mdogo wa Bunge, Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_34766" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi na upekuzi kwa watumishi wapya wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yaliyoanza leo, Dar es Salaam[/caption]

Na Mwandishi Wetu

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka watumishi wapya kuwa waadilifu na kutumia weledi katika kutekeleza majukumu yao ndani ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Dkt. Mafumiko amesema hayo leo wakati akifungua mafunzo elekezi na upekuzi kwa watumishi wapya arobaini na sita wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

“Taasisi hii inamajukumu makubwa kwa jamii na Serikali, hivyo mtumishi unapaswa kutumia weledi katika utekelekezaji wa majukumu yako na kuwa muadilifu na muaminifu katika kuyatekeleza majukumu utakayokabidhiwa.

[caption id="attachment_34764" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara, Bw. George Kasinga (kushoto) na Meneja Rasilimali Watu na Kumbukumbu, Bi. Nancy Nombo (kulia) wakiwa pamoja na watumishi wapya wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya ufunguzi wa mafunzo elekezi na upekuzi.[/caption]

Unapotumia taaluma yako katika kutekeleza majukumu ya kila siku fahamu unahusika moja kwa moja na maisha ya watu wengine, jamii na nchi, kwa sababu unahusika na usimamizi wa afya za binadamu na mazingira. Unapaswa kufahamu wewe kama mtumishi  ni kioo cha taasisi na Serikali, hivyo unapotumia weledi na uadilifu katika kutimiza majukumu yako ya kiuchunguzi wa kimaabara na kutoa majibu yenye kuaminika kwa jamii na Serikali inasaidia kukupa heshima kama mtumishi pamoja na taasisi na Serikali kwa ujumla.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali, aliwafahamisha watumishi hao kuwa majukumu yote yanayosimamiwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali yapo kisheria ndio maana inasimamia utekelezaji wa Sheria nne za nchi kwa sasa.

“Kila kinachotekelezwa na Mamlaka hii kipo kisheria, hivyo mtambue tunatekeleza majukumu ya Sheria nne ambazo ni Sheria inayoiunda Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Na.8 ya 2016, Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani Na. 3 ya mwaka 2003, Sheria ya Vinasaba vya Binadamu Na. 8 ya mwaka 2009 na Sheria ya Wanataaluma wa Kemia Na. 9 ya mwaka 2016, hivyo tunapaswa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Sheria hizo pia kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi