Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkemia Mkuu Awataka Madereva Kutumia Elimu Kuepusha Ajali za Kemikali
Jul 25, 2019
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_45745" align="aligncenter" width="750"] Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Usalama Barabarani Tanzania kutoka Jeshi la Polisi, Mrakibu, Abel Swai (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusu Utii wa Sheria Barabarani bila shuruti kwenye mafunzo ya madereva wanaosafirisha mizigo ya kemikali yaliyofanyika Dar es Salaam.[/caption]

Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko, amewataka madereva wanaosafirisha mizigo ya kemikali kutumia elimu waliyopata katika kuepusha ajali za kemikali ili kulinda afya za binadamu na mazingira.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya usafirishaji salama wa kemikali kwa madereva 36 kutoka kampuni zinazojihusisha na usafirishaji wa mizigo ya kemikali, Mkemia Mkuu wa Serikali amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu juu ya usafirishaji salama wa kemikali na misingi ya kufahamu kemikali ni hatari hivyo wanaposafirisha mizigo hiyo wanapaswa kuwa makini ili kulinda afya ya dereva mwenyewe, wananchi na mazingira anayopita.

[caption id="attachment_45746" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo (aliyesimama), akiongea kabla ya Mkemia Mkuu wa Serikali (katikati) hajafunga mafunzo hayo leo.[/caption]   [caption id="attachment_45747" align="aligncenter" width="750"] Mshiriki wa mafunzo kutoka Kampuni ya usafirishaji ya Alistair, Theobald Makanji (kushoto) akitoa neno la shukrani kabla ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufunga mafunzo hayo.[/caption]

“Napenda kuwapongeza sana kwa kuhudhuria mafunzo haya na kupata elimu kuhusiana na usafirishaji salama wa kemikali. Mnapaswa kufahamu lengo la mafunzo haya ni kuwapatia ufahamu juu ya usafirishaji salama wa mizigo ya kemikali kwa lengo la kulinda afya zenu, wananchi na mazingira mnayopita wakati wa kusafirisha kemikali. Nimefurahi kusikia kwa kauli zenu kama madereva kwamba mafunzo haya yamewabadilisha na kuwafanya kuwa madereva bora na makini zaidi, kwa sababu lengo la mafunzo pia ilikuwa ni kuwapatia uelewa kuhusu namna bora na salama ya usafirishaji wa kemikali na kwa kauli zenu wenyewe kuniambia kwamba mafunzo haya yamewabadilisha basi kwangu ni faraja kubwa kwani inanipa moyo wa matumaini na kunithibitishia kuwa timu iliyotoa mafunzo haya imefanikiwa kutimiza lengo.”

Aidha, Mkemia Mkuu wa Serikali aliwataka kutambua vyeti walivyopewa sio tu alama au pambo la kumaanisha wamemaliza mafunzo bali wakatumie elimu waliyopata kuwaelimisha madereva wengine ambao hawajafanikiwa kupata mafunzo kwa lengo la kuepusha ajali za kemikali na kulinda afya ya binadamu na mazingira.

“Vyeti mlivyopewa leo isiwe ni kama pambo au sifa tu ya kuonesha umepitia mafunzo kuhusu usafirishaji salama wa kemikali bali mnapaswa kuvitumia pamoja na elimu mliyopatiwa kusaidia kuepusha ajali za kemikali ikiwemo kuwaelimisha madereva wenzenu ambao hawajafanikiwa kupata mafunzo ili kulinda afya za binadamu na mazingira. Katika masuala ya maslahi yenu tutajitahidi kujenga ushawishi kwa ngazi nyingine zinazohusika pale tunapopata nafasi ili kuweza kufikisha kilio chenu.” Alimaliza.

[caption id="attachment_45748" align="aligncenter" width="750"] Madereva walioshiriki mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa.[/caption] [caption id="attachment_45749" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyesimama) akiongea wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya madereva wa makampuni yanayojihusisha na usafirishaji wa mizigo ya kemikali nchini na nje ya Tanzania yaliyofanyika katika Ukumbi wa TACAIDS, Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo na kushoto ni Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Maabara ya Kanda ya Mashariki na kuhusisha madereva thelathini na sita (36) kutoka makampuni mbalimbali.[/caption] [caption id="attachment_45750" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akikabidhi vyeti kwa wahitimu mara baada ya kukamilisha mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali leo.[/caption] [caption id="attachment_45751" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (kushoto), akikabidhi vyeti kwa wahitimu mara baada ya kukamilisha mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali leo.[/caption] [caption id="attachment_45752" align="aligncenter" width="750"] Mkemia Mkuu wa Serikali, Dkt. Fidelice Mafumiko (aliyekaa katikati), Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Kemikali, Daniel Ndiyo (kushoto) na Kaimu Meneja wa Maabara ya Kanda ya Mashariki, Danstan Mkapa (kulia) wakiwa pamoja na madereva waliohitimu mafunzo ya usafirishaji salama wa kemikali mara baada ya kukamilika mafunzo hayo leo kwenye ukumbi wa TACAIDS, Dar es Salaam.[/caption]

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madereva wenzake walioshiriki mafunzo hayo, Theobald Batholomeo Makanji, alisema mafunzo waliyopata ndani ya siku mbili hawakuyategemea na yamewabadilisha kiuwezo na wanajiona ni madereva wapya watakaofanyakazi kwa ufanisi mkubwa.

“Kwa niaba ya madereva wenzangu tunashukuru kwa mafunzo mazuri maana yametubadilisha na kutufanya kuwa madereva wapya. Sasa tunaelewa namna ya usafirishaji salama wa kemikali kuanzia kwenye maandalizi ya mzigo kupakia, kusafirisha na mpaka kushusha. Kemikali ni muhimu na ni hatari hivyo usafirishaji wake unapaswa kuwa na umakini ili ifike salama. Tumepata mafunzo katika hali ya weledi mkubwa na tumependa na tunaahidi kuwa mabalozi wazuri barabarani.”

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi