Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mkandarasi Atakiwa Kukamilisha Mradi wa Maji Chalinze Kufikia Desemba Mwaka huu
Oct 06, 2018
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_36389" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza katika eneo la utekelzaji wa mradi wa maji chalinze wakati wa ziara yake yakukagua hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo ambapo amemtaka mkandarasi kukamilisha mradi huo ifikapo Desemba 31, 2018. Na; mwandishi wetu[/caption]

Mkandarasi wa mradi wa maji Chalinze ametakiwa kukamilisha mradi huo kufikia mwezi Desemba mwaka huu ili wananchio waweze kupata huduma iliyokusudiwa ya maji safi na salama kama Serikali ilivyokusudia.

Akizungumza wakati wa ziara yake katika eneo la mradi huo, Mwenyekiti wa  Bodi ya Mamlaka hiyo Jenerali mstaafu Davis  Mwamunyange amesema kuwa mkandarasi huyo tayari ameshaongezewa muda mara 3 lakini bado ameshindwa kukamilisha mradi huo hivyo anatakiwa kukamilisha mradi huo katika katika muda huo.

" Mkandarasi ametueleza changamoto mbalimbali zinazomkabili ambazo kimsingi hazikubaliki na tunachotaka ni mradi huu ukamilike ifikapo Desemba 31 mwaka huu"; Alisistiza  Mwamunyange.

    [caption id="attachment_36390" align="aligncenter" width="750"] Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange ( katikati) akiendelea kukagua miundo mbinu inayojengwa katika chanzo cha maji cha mradi wa maji Chalinze kilichopo mto wami.[/caption]   [caption id="attachment_36391" align="aligncenter" width="900"] Mkuu wa Kitengo cha Mazingira na Msimamizi wa mradi wa maji Chalinze Mhandisi Modester Mushi akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange wakati alipotembelea mradi huo kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wake.[/caption] Akifafanua  amesema kuwa hatua mbalimbali zimechukuliwa na Serikali  katika kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika ili uweze kuwanufaisha wananchi. Utekelezaji wa mradi  huo utasaidia kuinua uchumi wa wananchi na kuchochea ujenzi wa uchumi wa viwanda  katika mkoa wa Pwani na maeneo ya jirani ya mkoa wa Tanga.

(Picha zote na DAWASA)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi