Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Tanzania Kuanza Kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Kiswahili
Oct 22, 2019
Na Msemaji Mkuu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kinapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa katika jitihada za kuikuza na kuieneza Lugha ya Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (CKD) kitaanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili.

Na hatua hii muhimu itaanza kutekelezwa rasmi kuanzia mwezi Januari 2020.

Mtakumbuka kwamba Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alishafanya jitihada kubwa sana na za kuiendeleza na kuieneza Lugha ya Kiswahili pamoja na kusimamia ubora wake ndani na nje ya nchi. Lakini hata Jitihada Marais waliofuatia katika awamu zote za uongozi wa nchi yetu pia walitilia sana mkazo suala hili la kukuza na kuiendeleza lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Katika awamu sasa tumeona mafanikio makubwa ya suala hili la kuiendeza lugha hii na sasa imekuwa ni moja kati ya lugha rasmi za Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika, yaani SADC. Na hii inatokana na msukumo mkubwa ambao umeonekana katika kipindi hiki cha Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Msukumo huu ukichangiwa na sababu nyingine umekifanya Kiswahili kuwa moja ya lugha kumi zenye wazungumzaji wengi duniani. Aidha kwa sasa lugha ya Kiswahili hinaundishwa katika shule na vyuo vikuu vingi hapa duniani.

Sasa Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukieneza Kiswahili na kusimamia ubora wake, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimechukua jukumu la kuanzisha mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kiswahili sanifu.

Ili lugha ya kimataifa ipate nguvu zaidi hutungiwa mitihani ili wanaojifunza lugha hizo waweze kutathminiwa na kupata vyeti.

Katika lugha kuu za dunia mitihani hii hufanyika ikiwa na majina mbalimbali. Kwa mfano:

  • mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa Lugha ya Kichina inajulikana kama HSK na HSKK;
  • Kihispaniola inajulikana kama DELE;
  • Kiingereza inajulikana kama TOEFL; na ya
  • Kiarabu inajulikana kama

CKD, kinakuwa ni Chuo Kikuu cha kwanza duniani kutunga mitihani hii na kusimamia utahini na usahihishaji wake na mwishowe kutoa Cheti cha Kimataifa kinachoonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa.

Ndugu Waandishi,

Ni ukweli ulio wazi kuwa CKD kina uzoefu wa kutosha na umahiri katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili na Vyuo Vikuu vingi hapa duniani vimekuwa vikipata uzoefu huo kutoka CKD.

Tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa CKD na walimu wanaofundisha Kiswahili katika vyuo vya nje kuhusiana na mitihani hii ambayo itaanza kutolewa mwakani.

CKD kimejiandaa kuhakikisha kuwa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iko madhubuti kuwezesha mitihani hii kufanyika kwa ufanisi na kwa viwango vya kimataifa. Kwani kuna wahitaji ambao watafanyia mitihani hii wakiwa katika nchi zao, sio lzima wasafiri na kuja kufanyia mitihani yao haoa Tanzania.

Walengwa wa mitihani hii ni watu wote ambao wanajifunza Kiswahili kama lugha ya pili au lugha ngeni katika ngazi mbalimbali ikilenga kupima usanifu katika kusoma; kuandika; kuongea; na kusikiliza.

Mitihani itafanyika mara sita kwa mwaka ikiendana na kipindi cha masomo ya Kiswahili kwa kila ngazi na itafanyika kwa njia za kielektroniki katika vyuo na vituo mbalimbali vya Kiswahili duniani ambavyo tayari kuna makubaliano maalumu kuhusu mitihani hii.

Katibu Mkuu

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

Kwa ushauri na ufafanuzi wasiliana na Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili kwa baruapepe hizi iks@udsm.ac.tz na dvc-arc@admin.udsm.ac.tz.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi