Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Michikichi Yawakomboa Wakulima Kigoma
Jun 03, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_52954" align="aligncenter" width="750"] Miche ya chikichi katika shamba la uzalishaji wa miche hiyo katika Kikosi cha 821 KJ Bulombora Kigoma ambapo miche 163,000 inazalishwa ikiwa katika hatua mbalimbali, huku miche 26,000 ikiwa tayari kupandwa katika shamba la kikosi hicho kufikia mwezi Oktoba 2020 ili kutekeleza azma ya Serikali kuwezesha Taifa kujitegemea kwa mafuta ya kula ambayo asilimia 60 kwa sasa inaagizwa kutoka nje ya nchi.[/caption]

Zao la michikichi ni moja ya mazao ya kimkakati ambayo yanalenga kuinua uchumi wa mtanzania na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu Majaliwa ameendelea kusema kuwa kwa Mkoa wa Kigoma tayari miche ya kisasa millioni 1, 800,000 imezalishwa na kuongeza kuwa tayari kituo cha utafiti  cha zao hilo la michikichi kimeanzishwa katika mkoa huo eneo la Kihinga jambo litakaloinua zao hilo na kuleta tija na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, Mkoa na Taifa kwa ujumla

Mkuu wa Kituo cha Utafiti TARI Kihinga, Dkt. Filson Kagimbo  amesema kuwa  Kituo hicho kinafanya kazi kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Jeshi la kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Magereza katika kuhakikisha kuwa azma ya Serikali inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Dkt. Kagimbo anasema kuwa Kituo hicho tangu maelekezo ya Waziri Mkuu kimeanza kuzalisha mbegu bora za michikichi ambazo kwa mujibu wa utafiti zinatoa mafuta mengi ikilinganishwa na za kizamani. Mbegu hiyo ni Tenera ambayo imeonekana kukua kwa muda mfupi na inatoa mafuta mengi na imependwa na wakulima wengi.

[caption id="attachment_52955" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya miche ya zao la mchikichi kama inavyoonekana katika kitalu cha uzalishaji wa miche hiyo katika Kikosi cha 821 KJ Bulombora Kigoma ambapo miche 163,000 inazalishwa ikiwa katika hatua mbalimbali, huku miche 26,000 ikiwa tayari kupandwa katika shamba la kikosi hicho kufikia mwezi Oktoba 2020 ili kutekeleza azma ya Serikali kuwezesha Taifa kujitegemea kwa mafuta ya kupikia ambayo asilimia 60 kwa sasa inaagizwa kutoka nje ya nchi.[/caption]

Kaimu Mkuu wa Kikosi cha 821 KJ Bulombora Kigoma, Meja. Victor Faustine Rutayuga  anasema kuwa miche 163,000 inazalishwa ikiwa katika hatua  mbalimbali, huku miche 26,800 ikiwa tayari kupandwa katika shamba la kikosi hicho kufikia mwezi Oktoba 2020 ili kutekeleza   azma  ya Serikali kuwezesha Taifa kujitegemea kwa mafuta ya kupikia.

Mnufaika wa Utafiti wa TARI, Bw. Raphael Daudi Baziliko anamshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka wakulima waliokuwa wa hali ya chini kwa kuwapelekea wataalaam wa kilimo cha michikikichi ambacho kimewaondolea umaskini.

[caption id="attachment_52956" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya miche ya zao la mchikichi kama inavyoonekana katika kitalu cha uzalishaji wa miche hiyo katika Kikosi cha 821 KJ Bulombora Kigoma ambapo miche 163,000 inazalishwa ikiwa katika hatua mbalimbali, huku miche 26,000 ikiwa tayari kupandwa katika shamba la kikosi hicho kufikia mwezi Oktoba 2020 ili kutekeleza azma ya Serikali kuwezesha Taifa kujitegemea kwa mafuta ya kupikia ambayo asilimia 60 kwa sasa inaagizwa kutoka nje ya nchi.[/caption]

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi