Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Gekul Amsihi Mrembo wa Tanzania 2022 Kuipeperusha Vyema Bendera ya Taifa
May 27, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Pauline Gekul, ametoa wito kwa Mlibwende wa Tanzania mwaka 2022 Halima Kopwe Kuipeperusha na kuitangaza vyema Tanzania ndani na Ulimwenguni kupitia taji alilonalo.

Naibu Waziri ametoa rai hiyo leo Mei 27, 2022 Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na mrembo huyo, katika mualiko aliompatia wa kulitembelea Bunge la Tanzania ili kuona shughuli za Bunge hilo.

"Wewe ndio umebeba jukumu la kuitangaza nchi yetu, umebeba Utamaduni wetu pamoja na lugha yetu adhimu ya Kiswahili, tunaamini utatangaza vyema vivutio vya Tanzania popote utakapokua na utakua Balozi mzuri kwa nchi yetu", alisema Mhe. Gekul.

Mhe. Gekul pia alimtaka mrembo huyo kudumisha nidhamu, huku akiitaka Kamati ya Miss Tanzania kumlea vyema mrembo huyo ili tasnia ya urembo iendelee kuheshimiwa zaidi na ivutie vijana wengi ambao wanatamani kuingia hatimaye Tanzania iwe kinara katika nyanja hiyo.

Kwa upande wake mrembo huyo, Halima Kopwe ameishukuru Serikali kwa mchango mkubwa inaoutoa katika kulea Sanaa na tasnia ya Urembo nchini, huku akiahidi Kuipeperusha vyema nchi katika kipindi chote atakachoshikilia taji hilo na baadae ambapo tayari ameingia kwenye rekodi za ulimbwende nchini.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi