Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Gekul Aiagiza BMT kuhakikisha TWFF Inafanya Uchaguzi
May 20, 2022
Na Jacquiline Mrisho

Na Shamimu Nyaki – WUSM, Dodoma

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul ameliagiza Baraza la Michezo Tanzania ( BMT) kuhakikisha Chama Cha Mpira wa Miguu Wanawake  nchini (TWFF) kinafanya uchaguzi ili wanawake wanaoshiriki michezo wapate uongozi utakaosaidia kuendesha michezo ya kundi hilo.

Naibu Waziri ametoa agizo hilo  leo Mei 20, 2022 alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) uliofika kujitambulisha kwa Naibu Waziri baada ya kufanya uchaguzi kwa ukamilifu.

"Hongereni sana kwa kufanya uchaguzi, Wizara tupo tayari kushirikiana na nyie katika kuendeleza netboli nchini, na nawaahidi wizara itakutana na nyie kuona mpango mkakati wenu wa kuendeleza mchezo huu," alisema Naibu Waziri Gekul.

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho, Rose Mkisi  alieleza kuwa CHANETA imepata uongozi bora unaozingatia miiko, uwazi, uwajibikaji na katiba katika kuongoza na kukuza mchezo wa netiboli nchini.

Uongozi wa chama hicho utadumu kwa muda wa miaka minne na umeainisha vipaumbele vyake ikiwemo kuibua vipaji  na kuviendeleza pamoja na uandaaji, usimamizi na uratibu wa mashindano katika ngazi mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi