Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mhe. Anastazia Wambura autaka Uongozi Wilaya ya Geita kushirikiana na Wasanii Filamu ya Magwangala katika kuiboresha.
Jul 29, 2017
Na Msemaji Mkuu

Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazi J. Wambura (aliyekaa mbele) akiongoza Kikao kilichowakutanisha Waandaaji wa Filamu ya 'Magwangala' (hawapo pichani) pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa wa Geita kwa ajili ya kutafuta namna ya kuiboresha filamu hiyo ili iweze kuvutiwa zaidi na Watanzania hivi karibuni alipotembelea Mkoani hapo.

Mbunge wa Geita Mjini, Mhe. Constantine J. Kanyasu (aliyesimama) akijibu baadhi ya hoja na kuchangia mada katika Kikao kwa ajili ya kuiboresha filamu ya Magwangala iliyoandaliwa na Wasanii wa Geita 28 Julai, 2017 Mjini Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Bw. Herman Kapuf (aliyesimama) akichangia mada katika Kikao kwa ajili ya kuiboresha filamu ya Magwangala iliyoandaliwa na Wasanii wa Geita 28 Julai, 2017 Mjini Geita.

Mfanyabiashara na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma (aliyesimama) akichangia mada kuhusu filamu ya Magwangala ambayo Mhe. Naibu Waziri Anastazia Wambura ameutaka Uongozi wa Wilaya kushirikiana na Waandaaji wa filamu hiyo kwa ajili ya kuioboresha zaidi.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi