Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Blogu ya Idara ya Habari - MAELEZO

Mfumuko wa Bei Washuka hadi asilimia 3.2
Jun 08, 2020
Na Msemaji Mkuu

[caption id="attachment_53080" align="aligncenter" width="750"] Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bi. Ruth Minja, akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwaka ulioishia Mei 2020, Mkutano huo umefanyika Ofisi ya Taifa ya Takwimu Jijini Dodoma.[/caption]

Na Mwandishi Wetu- Dodoma

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi  Mei, 2020 umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020.

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa  ya Takwimu (NBS), Bi. Ruth Minja, amesema kuwa hali hiyo  inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2020.

“Mfumuko wa  bei kwa bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula, mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Mei, 2020 umepungua hadi asilimia 4.4 kutoka asilimia 4.6 mwezi Aprili, 2020,” alisisitiza Bi.  Minja

 Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani kwa mwezi Mei, 2020 umebaki kuwa asilimia 5.2 kama ilivyokuwa mwezi Aprili, 2020.

Aliongeza  kuwa badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula kwa mwezi Mei, 2020 limepungua hadi asilimia 2.4 kutoka asilimia 2.5 mwezi Aprili, 2020.

 Mfumuko wa bei wa bidhaa na huduma zote usiojumuisha bidhaa za vyakula na nishati mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na nishati kwa mwezi Mei, 2020 umeongezeka kidogo hadi asilimia 2.2 kutoka asilimia 2.1 mwezi Aprili, 2020.

[caption id="attachment_53079" align="aligncenter" width="750"] Sehemu ya waandishi walioshiriki mkutano wa kutangaza kuhusu hali ya Mfumuko wa Bei kwa Mwaka ulioishia Mei 2020, Mkutano ulifanyika Ofisi za Takwimu Jijini Dodoma.[/caption]

 Fahirisi inayotumika kukokotoa aina hii ya mfumuko wa bei, haijumuishi vyakula vinavyoliwa nyumbani na migahawani, petroli, dizeli, gesi ya kupikia, mafuta ya taa, mkaa, kuni na umeme. Vyakula na bidhaa za nishati vina sifa ya kuwa na bei ambazo hubadilika mara kwa mara, hivyo vikiondolewa kwenye fahirisi ya bidhaa na huduma zote hubakia fahirisi ambayo ina mwelekeo imara kwa watunga sera.

Mwenendo wa fahirisi za bei za Taifa na mfumuko wa bei kutoka mwezi Mei, 2019 hadi Mei, 2020 unaonesha  kuwa, fahirisi za bei zimekuwa na mwenendo imara kutoka mwezi Mei, 2019 hadi mwezi Mei, 2020. Katika kipindi hicho, mfumuko wa bei ulikuwa kati ya asilimia 3.2 kwa mwezi Mei 2020 na asilimia 3.8 kwa mwezi Novemba na Desemba 2019.

Mabadiliko ya fahirisi za bei kati ya mwezi Aprili, 2020 na mwezi Mei, 2020 fahirisi za bei kati ya mwezi Aprili, 2020 na mwezi Mei, 2020 zimeongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.4 lililokuwepo kati ya mwezi Machi, 2020 na mwezi Aprili, 2020. Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 120.93 mwezi Mei, 2020 kutoka 120.67 mwezi Aprili, 2020.

Kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula. Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na: - mtama kwa asilimia 4.1, samaki kwa asilimia 3.0, dagaa kwa asilimia 1.2, karanga kwa asilimia 2.2, maharage kwa asilimia 5.7, mihogo kwa asilimia 2.6 and ndizi za kupika kwa asilimia 4.4.

Kwa upande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na: - bidhaa kwa ajili ya usafi wa kaya kwa asilimia 1.1, mavazi ya wanaume kama suti kwa asilimia 1.1, mavazi ya wanawake kama magauni kwa asilimia 1.3, kuni kwa asilimia 3.0, madaftari kwa asilimia 1.8 na gharama za saluni kwa wanawake kwa asilimia 1.1.

 

Mipangilio
Marekebisho ya Mandhari
Marekebisho ya Maandishi